Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Peter A, MD
Dkt. Benjamin M, MD
Jumatano, 9 Februari 2022

Kukua kwa tezi dume
Kukua kwa tezi dume hufahamika pia kama benine prostatic haipaplesia ni tatizo linalotokea kwa wanaume wenye umri mkubwa na huambatana na dalili mbalimbali zinazotokana na ongezeko la ujazo wa tezi. Tezi dume hujishughulisha na uzalishaji ute unaolisha na kusafilisha manii.
Dalili
Dalili za tezi dume iliyokuwa hutofautiana kati ya mtu na mtu na huongezeka makali kadri siku zinavyoenda. Dalili hizo ni;
Kukojoa mara kwa mara au hamu ya ghafla ya kwenda kukojoa
Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
Ugumu wa kukojoa
Mkojo kuwa na mkondo dhaifu ( mkojo kutoruka mbali) au unaokatika na kuanza tena
Matone ya mkojo kutoka wakati unapomaliza kukojoa
Kukosa uwezo wa kukojoa mkojo wote ulio ndani ya kibofu
Dalili za nadra zinajumuisha
Kupatwa na maambukizi ya UTI
Kushindwa kukojoa
Kukojoa mkojo uliochanganyika na damu
Ukali wa dalili mara nyingi huwa hautegemea ukubwa wa tezi. Baadhi ya wanaume wenye tezi kubwa huw ana dalili kiasi zaidi ya wale wenye tezi ndogo
Baadhi ya vitu vingine vinavyoweza kusababisha dalili kama za tezi dume ni
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)
Kuvimba kwa tezi dume kama matokeo ya shambulio la kinga ( prostaitiz)
Kusinyaa kwa mrija wa utoao mkojo nje ya mwili (urethra)
Makovu kwenye shingo ya kibofu cha mkojo
Mawe kwenye kibofu cha mkojo au figo
Madhaifu ya mishipa ya fahamu ya kibofu
Saratani ya tezi dume au kibofu cha mkojo
Wakati gani uwasiliane na daktari?
Kama una hisi una dalili hizi wasiliana na wataalamu wa afya mara moja ili kufanyiwa uchuguzi na kupata tiba. Hata kama unahisi kwamba dalili ni kiasi, usichelewe nyumbani ili kuepuka madhara ya tezi dume ambayo ni kuziba kwa njia ya mkojo inayoweza kupelekea kuferi kwa figo
Kisababishi
Nini husababisha kukua kwa tezi dume
Tezi dume imekaa chini kidogo ya kibofu cha mkojo na katikati yake imepitiwa na sehemu ya mwanzo ya mrija urethra unaotoa mkojo nje ya mwili. Tezi hii inapokua, huanza kubana mrija huo na kuzuia mkojo kupita vema.
Wanaume wengi tezi zao hukua kwa jinsi umri unavyoongezeka. Na kwa wanaume wengi tezi dume hukua kiasi cha kukandamiza au kuziba kabisa mrija urethra.
Haifahamiki kwa ujumla ni nini kinachosababisha tezi hii kukua, hata hivyo inafikiriwa ni kutokana na kupotea kwa uwiano wa homoni za kijinsia, hali inayotokea kwa jinsi umri unavyoongezeka
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupata tezi dume ni
Kuwa na umri mkubwa (Kwa nadra sana huweza kutokea kwa waanaume walio chini ya umri wa miaka 40. 1/3 ya wanaume kwenye umri wa miaka 60 hupata dalili za wastani kuelekea kuwa kali za tezi dume ilokuwa, na nusu ya wanaume wote wanapofkisha umri wa miaka 80 hupata dalili hizo)
Historia ya tezi dume kwenye familia mfano kaka au baba
Kuwa na kisukari au magonjwa ya moyo
Mtindo wa maisha ( kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi, kufanya mazoezi hupunguza hatari ya kukua kwa tezi dume)
Madhara ya tezi dume iliyokuwa
Madhara ni mara chache kutokea na hutokea endapo mtu hatapata tiba kwa wakati. Madhara hayo yanajumuisha
Kuziba kwa njia ya mkojo
Maambukizi ya UTI ya mara kwa mara
Kufanyika kwa mawe kwenye kibofu cha mkojo au figo
Uharibifu wa kibofu cha mkojo
Uharibifu wa figo
Uchunguzi
Huanza kwa kuulizwa maswali mbalimbali kasha kufanyiwa uchunguzi wa mwili na vipimo vingine vya damu, mkojo na kuangalia ukubwa wa tezi
Vipimo
Vipimo mbalimbali hufanyika kutazama ukubwa wa tezi na kutambua hali au magonjwa yanayoambatana, yanayofanana au yanayosababisha tezi dume. Baadhi ya vipimo vinavyofanyika ni;
Kipimo cha ultrasound
Vipindi cha mkojo
Kipimo cha homoni PSA
Vipimo vya uwezo wa kibofu kutunza na kusukuma
Kipimo cha kinyama cha tezi dume
Mtibabu
Matibabu ya tezi dume iiyokuwa hutegemea umri wa mtu, ukubwa wa tezi, ukali wa dalili, na hali ya afya ya mgonjwa.
Matibabu yanaweza kuhusisha matumizi ya dawa au upasuaji
Tiba mbadala
Baadhi ya tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa kuna baadhi ya mimea ambayo inauwezo wa kusinyaza tezi dume iliyokuwa na hivyo kupunguza dalili zake. Usalama wa matumizi wa dawa hizo kwa muda mrefu bado haujathibitishwa.
Kujitibu nyumbani
Mambo unayoweza kufanya nyumbani kama una tezi dume
Dhibiti kiwanfo cha vinywaji unavyokunywa (usinywe maji lisaa moja kabla ya kwenda kulala usiku)
Usinywe pombe au vinywaji vyenye kafeini kuzuia kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
Dhibiti kiwango cha dawa jamii ya histamine kwani hudhibiti misuli ya kibofu na kufanya ushindwe kukojoa kirahisi
Nenda msalani mara unapohisi haja ndogo
Kuwa na ratiba ya kukojoa, mfano kila baada ya masaa 4 hadi sita ili kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo wako
Kula mlo wa kiafya na dhibiti uzito kwenye kiwango kinachotakiwa
Ukimaliza kukojoa, kojoa tena ili kutoa mkojo uliobaki kwenye kibofu
Fanya mazoezi ili kusaidia mkojo kutobaki kwenye kibofu
Hakikisha unaupa mwili joto kama unaishi maeneo yenye baridi ili kuzuia kibofu kutunza mkojo muda mrefu