Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Peter A, MD
Mhariri: Sospeter B, MD
Jumanne, 16 Mei 2023
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo kadha wa kadha, visababishi kama gesi kujaa tumboni, ama mijongeo ya misuli ya tumbo huwa havina madhara sana. Visababishi mbali na hivyo huhitaji matibabu yafanyike kwa haraka.
Â
Mara nyingi, sehemu maumivu yalipo yanaweza kuelezea kisababishi cha maumivu hayo. Wakati mwingine, maumivu ya tumbo yanaweza kutokea katika namna ya kutoeleweka na kutofahamika sababu inayosabisha maumivu hayo. Hata hivyo ni jambo la msingi kujua sababu ya maumivu ya tumbo kutokana na mahali maumivu hayo yalipo katika tumbo lako.
​​
Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mijongeo ya misuli ya tumbo huwa ya muda mfupi na huwa si ya hatari sana.
​
Maumivu makali ya tumbo humaanisha kuna hali au ugonjwa wa kutiliwa umaanani sana, maumivu hayo yakianza ghafla na bila kutarajiwa hutakiwa kutibiwa kwa dharura haswa endapo maumivu hayo yamejikita sehemu moja ya tumbo au matumbo.
Â
Endapo unapata maumivu hayo makali, piga namba za simu kwa matibabu ya harakakutoka kwa daktari au mamlaka zilizo karibu na wewe au wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa haraka wakati unafanya mpango wa kufika hospitali
Â
Sifa za maumivu ya tumbo
​
Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa yenye sifa kadhaa kama vile;
​
Maumivu ya kuungua na moto
Kunyonga
Kukata
Kung’ata
Maumivu makali sana
Maumivu ya kuchoma na kitu
Maumivu sugu
Maumivu yanayoongezeka jinsi muda unavyokwenda
Maumivu ya kuja na kuondoka
Â
Licha ya kuwa na sifa tofauti maumivu ya tumbo yanaweza pia kuwa sehemu mbalimbali za mwili, maumivu katika sehemu hizi mbalimbali huashiria kuna shida katika sehemu hiyo. Maeneo ambayo maumivu ya tumbo yanaweza kutokea ni;
​
Maumivu yanayoanzia tumboni na kuhamia sehemu nyingine za mwili
Maumivu ya chini ya kitovu
Maumivu ya katikati ya tumbo
Maumivu upande mmoja wa tumbo
Maumivu juu ya kitovu
​
Licha ya kuwa katika sehemu fulani ya mwili, maumivu ya tumbo pia yanaweza kuamshwa na;
​
Kukohoa au kutembea
Kunywa pombe
Kula vyakula aina Fulani
Msongo wa mawazo
Hedhi
​
Kwa baadhi ya watu maumivu ya tumbo huweza kufisha au kuamsha na vitu au mambo kadhaa ambayo ni vema kufahamu ili uweze kumwambia daktari wako na kumsaidia kujua shida ni nini, vitu hivyo ni;
​
Kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kama omeprazole, lansoprazole
Kuacha kula vyakula aina fulani
Kubadili pozi la mwili
Kula vyakula aina fulani
Kula mboga za majani kwa wingi
Â
Kuna hali au mambo mbalimbali yanayoweza kuambatana na maumivu ya tumbo, ni muhimu pia kuyafahamu na kumwambia daktari wako, daktari wako pia atakuuliza pia mambo hayo ili kukua tatizo lako haswa ni nini, mambo hayo ni;
​
Kuvimba kwa tumbo
Kupata choo cheusi au chenye damu
Haja ngumu
Kuharisha
Homa
Kushindwa kutoa haja kubwa licha ya kuwa na hamu ya kujisaidia
Kupata Choo kilaini chenye majimaji
Kichefuchefu na kutapika
Kijambo chenye arufu mbaya
Kuhisi mdundo wa mishipa ya damu karibia na kitovu
Harara kwenye ngozi
Matumbo kupiga kelele
Kupoteza uzito bila sababu
Uhiaji wa kwenda haja kubwa mara moja
Â
Visababishi
 Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo kama ilivyoelezewa kutokana na sifa za maumivu hayo ya tumbo na sehemu/mahali yalipo au ni nini kichachoyafanya yapoe au kuwa makali Zaidi.
​
Baadhi ya visababishi vimeorodheshwa hapa chini, kumbuka mada hii itaendelea kuongezwa visababishi vingine ambavyo havijaorodheshwa hapa.
Â
Maumivu ya ghafla ya kunyonga yanayoambatana na kuharisha
 Endapo maumivu yameanza hivi karibuni na yanaambatana na kuharisha, kisababishi kinaweza kuwa maambukizi kwenye mfumo wa tumbo kwa jina tiba gastroenteritis. Maambukizi haya yanaweza kuwa ya bakteria au virusi kwenye matumbo au tumbo, kumbuka maumivu haya yatapona bila matibabu ndani ya siku chache
Â
Ugonjwa wa gastroenteritis unaweza kusababishwa na kula chakula chenye sumu au kula chakula kilichochanganyika na kinyesi cha mtu mwenye tatizo hilo. Chakula hiki kinaweza kuwa kimeandaliwa na mtu mwenye tatizo hili au kutumia maji yaliyochanganyika na kinyesi cha mtu mwenye tatizo.
​
Kama unapata maumivu mara kwa mara na kuharisha, unawez akuwa na tatizo la muda mrefu la sindromu ya Iritabo baweli
Â
Maumivu makali na ya ghafla
 Kumbuka endapo una maumivu aina hii wasiliana na daktari wako kwa huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo.
​​
Kama una maumivu makali sana na ya ghafla, ni dhahiri unaweza kuwa kuna sababu ya hatari inayohitaji matibabu ya haraka. Maumivu hayo yanaweza kusababishwa na;
​
Homa ya kidole tumbo– hili ni tatizo la kuvimba kwa kidole tumbo kutokana na maambukizi. Husababisha maumivu chini ya kitovu upande wa kulia. Endapo shida ipo kwenye kidole tumbo inamaanisha kinatakiwa kutolewa kwa upasuaji.
Kutoboka kwa tumbo- kama kuna kidonda ndani ya tumbo au ulikuwa na vidonda vya tumbo, vinaweza kutoboka na kusababisha damu kuvilia ndani ya utumbo. Hii inaweza kuleta maumivu makali sana ya tumbo yasiyoweza kupoa kirahisi na huweza kuambatana na kuvimba kwa tumbo na kutokwa jasho jingi au kuzimia, kutokwa na kinyesi cheusi kabla dalili hii kutokea.
Kolesistaitiz kali- hii husababishwa na michomo kwenye kifuko cha nyongo inaotokana na kufanyika kwa mawe ndani ya kifuko hiko. Utatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kifuko hiki
Mawe kwenye figo- kufanyika kwa mawe ndani ya figo au katika mirija ya figo huweza kuziba njia ya mkojo, utatakiwa kufika hospitali mara moja ili njia hizo zizibuliwe kuepuka uharibifu wa mirija ya mkojo na figo
Homa ya vifuko kwenye utumo mpana- hutokana na michomo kwenye vifuko vilivyo kwenye utumbo mpana, michomo hii hutokea kwa sababu ya maambukizi kwenye vifuko hivi. Utahitaji kupatiwa tiba dawa.
Maumivu ya tumbo baadhi ya nyakati yanaweza kusababishwa na sababu ambazo zinatibika kama vile maambukizi au sababu ambazo zinaisha zenyewe kama kujongea kwa misuli
Â
Maumivu ya tumbo ya muda mrefu au ya kujirudia
 Maumivu ya tumbo ya muda mrefu na ya kujirudia mara nyingi huwa si ya hatari sana, onana na daktari ili kujua kisababishi ni nini na kupata tiba.
Â
Baadhi ya visababishi ni
Â
Sindromu ya inflamatory bawel- ugonjwa huu huambatana kunyonga kwa tumbo, kuharisha au haja ngumu. Maumivu yanapoa baad aya kujisaidia
Ugojnwa wa inflamatori baweli huhusisha magonjwa mawili ambayo ni ugonjwa wa Crohn's na  asaletivu kolaitizi, hata hivyo ugonjwa wa endometriosisi pia huweza kusababisha aina hii ya maumivu
Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo(UTI)- maumivu haya huwez akujirudia rudia kw abaadhi ya watu, utapata dalili zifuatazo pia, kuungua wakati w akukojoa, kuwa au kutokuwa na homa, kichefuchefu, kutapika.
Haja ngumu- huweza kutokea na kusababisha maumivu ya tumbo, huambatana na mabadiliko ya hedhi pia
Â
Matatizo mengine ya tumbo
Vidonda vya tumbo
Kiungulia
Kucheua tindikali na
Ugonjwa wa gastraitizi
Â
Maumivu ya tumbo kwa watoto yanaweza kusababishwa na;
Â
Haja ngumu
UTI
Kiungulia na Kucheua tindikali
Kipand auso cha tumbo
​
Soma zaidi kuhusu maumivu ya tumbo kwa mwanamke, bonyeza hapa