top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULYCLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

Alhamisi, 1 Julai 2021

Saratani

Saratani

Kufahamu saratani ni nini ni vema kwanza kufahamu kuwa mwili wa binadamu umetengenezwa kwa chembe hai zenye uwezo wa kuzaliana, kukua na kufa mara zinapozeeka au zinapopoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Utaratibu huu ni wa asili na huongozwa na vimeng’enya maalumu vilivyo ndani ya chembe hai ambayo hurithiwa kwenye jeni. Endapo jeni ya chembe moja itabadili utaratibu huu kutokana na sababu yoyote na kuanza kuzalina kwa haraka, kuishi bila kufa na kutengeneza uvimbe sehemu husika ya mwili hii husababishwa kutokea kwa saratani.

Dalili


Kama ilivyo kawaida ya magonjwa mengine kutoonesha dalili za haraka mwanzoni, vivyo hivyo dalili za saratani ni vigumu kuonekana mara inapoanza na hivyo kufanya kuwa rahisi kuchelewa kutambuliwa.


Endapo dalili zitaanza kuonekana, zitategemea sehemu saratani ilipo au sehemu imejipandikiza baada kusambaa na huongezeka kwa jinsi tatizo linavyozidi kuwa kubwa.


Dalili za saratani zinajumuisha;


 • Uchovu mkali

 • Uvimbe eneo ambapo kuna ssaratani

 • Kupungua uzzito bila sababu

 • Mabadiliko ya ngozi kama vile kuwa nyeusi zaidi au nyekundu zaidi n.k

 • Mabadiliko ya tabia ya tumbo

 • Kukohoa endelevu au kukuhoa damu

 • Mabadiliko ya tabia ya kukojoa

 • Kushindwa kumeza chakula

 • Kukwa ma kwa sauti ( sauti ya farasi)

 • Kutokwa na damu ukeni

 • Difficulty swallowing

 • Kutokwa na damu bila sababu

 • Maambukizi ya mara kwa mara

 • Maumivu ya viungo yasiyo na sababu


Visababishi


Saratani husababishwa na mabadiliko yanayotokea kwenye jeni ya seli, ambayo hupelekea seli kupoteza uwezo wake wa kujizalisha, kukua na kufa kwa utaratibu wake wa awali.


Ni nini husababishwa mabadiliko ya jeni za chembe hai?

 • Mabadiliko ya kuzaliwa nayo. Haya hurithiwa kutoka kwa wazazi, saratani aina hii hutokea kwa asilimia chache.

 • Mabadiliko ya jeni baada ya kuzaliwa

 • Mabadiliko ya jeni husababishwa na;

 • Uvutaji wa sigara

 • Kupigwa na mionzi

 • Maambukizi ya virusi

 • Matumizi ya kemikali zinaofahamika kuwa kasinojeni

 • Uzito uliokithiri

 • Michomo sugu ya kinga za mwili

 • Kutofanya mazoezi


Aina za saratani


Saratani inaweza kujitokeza sehemu yoyote ile ya mwili wa binadamu, sehemu saratani ilipo au aina ya tishu zilizoathiriwa huipa jina la saratani. Mfano wa saratani zinazotokea ni saratani ya;


 • Damu

 • Ini

 • Kibofu cha mkojo

 • Kongosho

 • Koo

 • Macho

 • Mapafu

 • Matiti

 • Mifupa

 • Misuli

 • Ngozi

 • Shingo ya kizazi (seviksi)

 • Tezi dume

 • Tezi limfu

 • Tumbo

 • Ubongo

 • Utumbo


Vihatarishi


Mara nyingi haifahamiki ni nini kinatokea hadi chembe hai kuwa na tabia isiyo ya kawaida na kuleta saratani. Wanasayansi wameona kuwa kuna mchanganyiko wa mambo mengi ambayo kwa pamoja yanaweza kupelekea kupata saratani. Licha ya sababu kutofahamika, vipo vihatarishi vinavyofahamika kusababisha saratani endapo mtu atakuwa navyo ambavyo ni;


 • Matumizi ya kemikali kali

 • Kupigwa na mionzi

 • Uvutaji wa sigara

 • Maambukizi ya virusi virus , bacteria na fangasi

 • Matumizi ya pombe kupindukia

 • Ulaji wa vyakula vya mafuta mengi

 • Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi

 • Kutofanya mazoezi

 • Unene uliokithiri

 • Matumizi ya dawa mbalimbli au viua wadudu

 • Kuanza ngono kwenye umri mdogo au kuwa na wapenzi wengi


Chembe za saratani zinaweza sambaa?


Chembe za saratani zinauwezo wa kusafiri kutoka sehemu moja ya mwili kwenda nyingine kwa kupitia;


 • Njia ya damu

 • Njia ya limfu

 • Njia ya kupenyeza chembe jirani


Saratani inaambukizwa?


Hapana! Saratani haiambukizwi


Vipimo na utambuzi


Saratani hutambuiwa kwa njia tofauti zikiwa pamoja na;


Uchunguzi wa mwili wako na daktari

Daktari atchunguza uvimbe baada ya kuchukua historia ya tatizo lako kwa kutumia mikono au vifaa mbalimbali vya kitaalamu ili kutambua kama una saratani na sifa zake.


Vipimo vya picha ya mionzi

Vipimo hivi hufanyika kutambua aina na sifa za saratani na maeneo ambapo saratani imesambaa vipimo hivyo hujumuisha


 • Computerized tomography (CT) scan,

 • Bone scan,

 • Magnetic resonance imaging (MRI)

 • Positron emission tomography (PET) scan

 • Ultrasound

 • X-ray

 • Na vingine


Kipimo cha biopsy

Chembe za saratani zitachukuliwa kwa ajili ya kutizama uwepo wa saratani kwenye chembe hizo maabara, hii ni njia pekee inayoweza kusema kutofautisha uvimbe wa kawaida na saratani. Utambuzi wa saratani kwa njia hii hutumia kuangalia sifa za chembe za saratani na sehemu zilipotoka, endapo chembe zitaonekana kuwa zina maumbile tofauti ya sehemu zilipotoka na hazina mpangilio mzuri, chembe hizi huwa na sifa ya saratani.


Vipimo vya maabara

Vipimo vya mkojo na damu hufanyika kwa lengo la kutambua saratani au madhara ya saratani. Mfano wa vipimo ni FBP ambacho hufanyika sana kwa wagonjwa wenye saratani ya damu.


Matibabu


Matibabu ya saratani yapo ya aina nyingi ikitegemea aina ya saratani na mahali ilipo katika mwili. Daktari anaweza kupendekeza matumizi ya tiba moja au zaidi ya moja, na huhusisha;


 • Upasuaji wa kuondoa uvimbe au sehemu ya uvimbe

 • Dawa za chemotherapi

 • Tiba ya kutumia Mionzi kuua chembe za saratani

 • Tiba ya vichochezi au homoni

 • Tiba dhamiria- hulenga kutambua udhaifu wa chembe za saratani unaofanya chembe iwe na tabia za kisaratani kisha kuzuia

 • Tiba ya jeni- hulenga kutambua udhaifu wa jeni

 • Tiba ya stem seli

 • Tiba majaribio- hizi ni tafiti zinazolenga kugundua dawa mpya za saratani, kuna tafiti nyingi zinaendelea duniani kudungua njia nzuri na mpya za matibabu ya saratani.


Tiba mbadala ya saratani

Hakuna tiba mbadala (tiba asilia) ambayo imethibitishwa kutibu saratani, hata hivyo kuna baadhi ya dawa asili zimeonekana kutibu saratani na baadhi ya wagonjwa wamepona kwa kutumia tiba hizo. Unapokuwa unatumia tiba mbadala unatakiwa kushauriana na daktari wako kwanza kuhusu mwingiliano wa tiba hizo na dawa za hospitali.


Kuna matibabu ya kuponya saratani?

Jibu la swali hili kwa sasa ni hapana, hii ni kwa sababu hakuna tiba mpaka sasa iliyothibitishwa kuponya saratani kabisa. Hata hivyo kuna matibabu ya kupunguza au kudhibiti saratani na endapo itagunduliwa mapema kwenye hatua za awali kabisa, mwathirika anaweza kupona na hivyo kuishi na kufa na magonjwa mengine yasiyohusiana na saratani kama watu wengine.


Matibabu mengi yaliyopo hayaponyi saratani bali humponya mtu kwenye madhara ya saratani lakini saratani huendelea kuwa kisababishi cha kifo kwa waathirika haswa endapo waligunduliwa kwa kuchelewa.


Kinga

Baadhi ya saratani ambazo zinazofahamika visababishi vyake huweza zuilika kwa kufanya mamb yafuatayo;


Acha kuvuta sigara

Kama unavuta sigara unapaswa kuacha ili kujikinga na saratani ya mapafu na zingine zinazotokana na uvutaji wa sigara.


Jikinge na kupigwa na mwanga wa jua kupita kiasi

Mwanga wa jua una mionzi ambayo inaweza kupelekea kupata saratani ya ngozi. Kaa kwenye kimvuli muda mwingi au kuvaa nguo au kupaka mafuta ya kukukinga na mionzi haswa endapo una ualbino


Kula mlo wa kiafya

Kula mlo kamili wa kiafya unaopendekezwa haswa wenye mboga za majani kwa wingi na nafaka zisizokobolewa. Usile nyma yenye mafuta au nyama nyekundu kwa wingi.


Fanya mazoezi

Inashauriwa kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30 kwa muda wa siku 3 hadi 4 kwa wiki. Fanya mazoezi ya aerobiki na anaerobic


Kuwa na uzito wa kiafya

Zingatia kuwa na BMI inayoshauriwa kwa kuzingatia mlo na kufanya mazoezi


Kunywa pombe kidogo

Kama umechagua kunyw apombe, kunywa kwa kiasi kidogo kinachoshauriw akiafya kwa siku.


Fanya uchunguzi wa saratani

Ongea na daktari wako akufahamishe unatakiwa kuanya uchunguzi wa saratani gani kulingana na kihatarishi ulichonacho.


Pata chanjo ya saratani zilizopo

Kuna chanjo nyingi zipo kama vile chanjo ya kirusi cha homa ya ini B (HBV) anayesababisha saratani ya ini, kirusi cha human papillomavirus (HPV) anayesababisha saratani ya shingo ya uzazi na koo na zingine.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

26 Oktoba 2021 21:04:55

Rejea za mada hii:

1. How cancer starts, grows and spreads. https://www.cancer.ca/en/cancer-information/cancer-101/what-is-cancer/how-cancer-starts-grows-and-spreads/?region=on. Imechukuliwa 1/07/2021

2. LONG LI, et al. Metastatic nerve root tumor: A case report and literature review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4887964/. Imechukuliwa 1/07/2021
3. Cancer. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/cancer/symptoms-causes/syc-20370588. Imechukuliwa 1/07/2021

4. . Cancer.Net. How cancer is treated. https://www.cancer.net/navigating-cancer-care/how-cancer-treated. Imechukuliwa 30.01.2021

5. Cancer stat facts: Cancer of any site. National Cancer Institute Surveillance, Epidemiology, and End Results Program. https://seer.cancer.gov/statfacts/html/all.html. Imechukuliwa 30.01.2021

6. Cancer.Net . Making decisions about cancer treatment. https://www.cancer.net/navigating-cancer-care/how-cancer-treated/making-decisions-about-cancer-treatment. Imechukuliwa 30.01.2021

7. National Cancer Institute .Cancer staging. https://www.cancer.gov/about-cancer/diagnosis-staging/staging. Imechukuliwa 30.01.2021

8. National Cancer Institute. Cancer prevention overview (PDQ) — Health professional version. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/hp-prevention-overview-pdq. Imechukuliwa 30.01.2021

9. National Cancer Institute. Cancer screening overview (PDQ) — Health professional version. https://www.cancer.gov/about-cancer/screening/hp-screening-overview-pdq. Imechukuliwa 30.01.2021

10. National Cancer Institute. How cancer is diagnosed.. https://www.cancer.gov/about-cancer/diagnosis-staging/diagnosis. Imechukuliwa 30.01.2021

11. National Cancer Institute. Symptoms of cancer. https://www.cancer.gov/about-cancer/diagnosis-staging/symptoms. Imechukuliwa 30.01.2021

12. National Cancer Institute. Taking time: Support for people with cancer. https://www.cancer.gov/publications/patient-education/taking-time. Imechukuliwa 30.01.2021

13. National Cancer Institute. What is cancer? https://www.cancer.gov/about-cancer/understanding/what-is-cancer. Imechukuliwa 30.01.2021

14. Niederhuber JE, et al., eds. Genetic and epigenetic alterations in cancer. In: Abeloff's Clinical Oncology. 6th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 30.01.2021

15. Paraneoplastic syndromes information page. National Institute of Neurological Disorder and Stroke. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/All-Disorders/Paraneoplastic-Syndromes-Information-Page. Imechukuliwa 30.01.2021

16. Rock CL, et al. American Cancer Society guideline for diet and physical activity for cancer prevention. CA: A Cancer Journal for Clinicians. 2020;doi:doi.org/10.3322/caac.21591.

17. The genetics of cancer. National Cancer Institute. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/genetics. Imechukuliwa 30.01.2021

18. Ulcerative colitis. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/ulcerative-colitis/all-content. Imechukuliwa 30.01.2021

19. Understanding cancer risk. Cancer.Net. https://www.cancer.net/navigating-cancer-care/prevention-and-healthy-living/understanding-cancer-risk. Imechukuliwa 30.01.2021

20. World Health Organization. Cancer.. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/cancer. Imechukuliwa 30.01.2021

21. Web md. Is There a Cure for Cancer?. https://www.webmd.com/cancer/guide/cure-for-cancer. Imechukuliwa 30.01.2021

bottom of page