top of page
Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 5 Novemba 2021

Vidonda kwenye ulimi
Vidonda kwenye ulimi huweza kuonekana Kama vijishimo vidogo vyenye rangi nyeupe au njano kwenye ulimi au kwenye fizi chini kidogo ya meno.
Visababishi
Vidonda hivi huitwa canker, huwa haviambukizwi na mara nyingi husabaishwa na vitu tunavyotumia kila siku kama kemikali kwenye dawa za miswaki, dawa za kuosha mdomo, mzio wa chakula, au upungufu wa vitamin aina fulani mwilini. Wakati mwingine hakuna kisababishi kinachojulikana kusababisha vidonda hivi.
Visababishi vingine
Visababishi vingine vya maumivu ya ulimi huwa pamoja na;
Saratani
Upungufu wa damu
Maambukizi ya virusi vya Herpes
Kuvaa vidani kwenye ulimi
Matatizo ya mishipa ya fahamu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba, au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
13 Julai 2023 19:03:22
Rejea za mada hii:
bottom of page