Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Benjamin L, MD
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 28 Oktoba 2021

Vipele mshikizo
Vipele mshikizo ni vipele vidogo vinavyoning’inia juu ya ngozi. Vipele hivi huwa havina shida yoyote, hupatikana kwenye maeneo ya shingo, kufuani, mgongoni, na kwapani. Hutokea sana kwa wanawake haswa wanaoongezeka uzito sana na watu wazima.
Vipele mshikozo huwa havisababishi maumivu mara nyingi, hata hivyo huweza kubadilika na kuleta maumivu endapo vimegusana na kitu chochote kama kidani, Mafuta, kupata msuguano n.k
Hutibiwaje?
Daktari wa Ngozi anaweza kutibu vipele mshikizo kwenye Ngozi kwa kufanya upasuaji mdogo wa kukata na kisu cha upasuaji au kutumia kisu cha umeme au njia ya kugandisha kipele au dawa.
Kulinda ngozi yako fanya mambo yafuatayo;
Acha kukaa kwenye jua kali
Sehemu nyingi za dunia hasa kwenye ukanda wa tropic kuna jua kali, jua huwa na mionzi ambayo inaathiri Ngozi. Licha ya jua la asubuhi kusaidia kutengeneza Vitamini D, jua la mchana huwa na athari ya kuweza kusababisha daratani ya Ngozi hasa kwenye mabaka haya meusi
Tumia losheni za kujikinga na mionzi ya jua mwaka mzima
Paka losheni hii dakika 30 kabla ya kwenda kwenye mwanga mkali wa jua, hata kama kuna mawingi na mvua.
Funika maeneo ya mwili wako
Tumia miwani maalumu ya kuzuia mwanga wa jua utakayopewa na daktarin wako. Kofia za kusambaa(hats) nguo za mikono morefu, na nguo zingine ambazo zinaweza kuzuia kupigwa na mionzi hatari ya jua. Unaweza kuvaa nguo maalumu zilizotengenezwa kwa ajili ya kazi ya kukinga na mionzi ya jua.
Achana na taa au vitanda vinavyotoa mwanga wa UV.
Vitanda hivi au taa aina hizi zinazotoa mwanga wa Ultraviolent huongeza hatari ya kupata saratani ya Ngozi. Tafiti zinonyesha kuuweka mwili kwenye mwanga huu mara moja tu kunaongeza hatari mara 26 zaidi ya kupata saratani ya Ngozi.