Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Salome A, MD
Dkt. Benjamin L, MD
Jumapili, 2 Julai 2023

Wasiwasi wa kiharusi mpito
Wasiwasi baada ya kiharusi cha mpito ni bakia la dalili linalotokea kwa waathiriwa wengi wa kiharusi cha mpito na kiharusi kidogo. Aina ya wasiwasi unaotokea sana ni ule wa woga usio kawaida au kuepuka jambo ambapo kitiba hufahamika kama fobia pamoja na wasiwasi wa jumla.
Wasiwasi kwa baada ya kiharusi cha mpito huambatana na matokeo hasi kwa mwathirika zinazoweza kuzuilika kwa kuchukua hatua kabla ya kutokea kwa kutambua mapema kwamba kuna dalili hii.
Matibabu ya wasiwasi bada ya kiharusi yanapaswa kuzigatia aina mbalimbali za matibabu ili kulenga kutibu woga na wasiwasi wa jumla.
Wasiwasi wa woga
Wasiwasi wa woga sifa zake ni kuwa na wasiwasi usio wa kawaida kwenye jambo linaloeleweka. Mhusika akiwekwa kwenye kiamsha wasiwasi dalili mbalimbali za wasiwasi zinazoambatana na tabia ya kuepuka jambo linalosababisha wasiwasi hutokea.
Licha ya tabia ya kuepuka kiamsha wasiwasi inaweza kuzuia wasiwasi kwa muda mfupi, inaweza kuwa na athari kubwa ikitumika mara kwa mara kama njia ya kutatua tatizo. Mfano kukaa ndani kwa sababu ya wasiwasi wa kukosa msaada endapo utapatwa na jambo ukiwa nje ya nyumba inaweza kuwa na athari nyingi kwa mgonjwa na wanaomzunguka.
Matibabu ya wasiwasi wa woga yanahitaji kufanyika kwenye mpangilio mzuri wa kujianika katika visababishi hatua kwa hatua.
Wasiwasi wa jumla huwa sambavu na endelevu na huwa na sifa ya woga endelevu kwenye jambo Zaidi ya moja mfano, fedha, afya na kukosa uwezo wa kuacha kuhofu.
Matumizi ya dawa za wasiwasi, tiba ya akili huwa na matokeo mazuri kwenye matibabu ya wasiwasi wa jumla.
Bofya hapa kwenda kwenye makala ya tiba takatifu ya kiharusi mpito