top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Kuishi maisha ya ngono na mwathirika wa VVU

 

Licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana dhidi ya kupambana na madhara makubwa ya VVU, ugonjwa wa UKIMWI umeendelea kuwa mzigo mkubwa sana kwenye jamii nyingi duniani. Suala ambalo limezuka baada ya kudhibiti makali ya maambukizi ya VVU ni kutokea kwa mahusiano ya kingono kati ya mtu ambaye hana maambukizi na mwathirika wa VVU, suala hili linatakiwa kufahamika na jamii ili kujua ni namna gani wapenzi hawa waishi na kuondoa hatari ya kuambukizana au kuwaambukizi watoto wanaozaliwa na mzazi mmoja aliyeathirika na Virusi vya UKIMWI.

 

Wapenzi wengi mara baada ya kupima hali ya maambukizi na mmoja kufahamika kuwa na VVU, mahusiano hayo huvunjika mara moja. Hata hivyo baadhi mara baada ya kupokea elimu kutoka kwa wataalamu wa afya huendeleza mahusiano yao na hivyo huweza kuishi kama kawaida pasipo mpenzi asiye na VVU kupata maambukizi hayo.

 

Makala hii ni mahususi kuzugumzia kuhusu maisha ya mahusiano ya kingono kati ya mwathirika wa VVU na mpenzi wake ambaye hana maambukizi hayo.

 

Utangulizi

 

Maambukizi ya UKIMWI ni maambukizi yanayoambukizwa sana kwa njia ya ngono, na pia ikifuatiwa na njia ya mama kwenda kwa mtoto. Njia hizi mbili ni lazima kueleweka vema kwa wapenzi wawili ambao wanatofauti za kimaambukizi yaani mpenzi mmoja kuwa na maamvukizi na mwingine kutokuwa na maamvukizi hayo.

 

Vitu gani vya kuzingatia kwa wapenzi ambao wanautofauti wa hali ya maambukizi ya VVU?

​

Ili wapenzi wawili wenye utofauti wa hali ya maambukizi ya VVU waweze kuishi maisha yao mazuri bila ya kusafirisha maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni vema wakazingatia ushauri huu kama utakavyoshauriwa na daktari wako.

​

Tumia kondomu wakati wa kushiriki ngono

 

Matumizi sahihi ya kondomu hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya VVU. Matumizi ya kondomu wakati wa kutafuta mtoto hayashauriwi, lakini kipindi hiki ni lazima kufuata ushauri wa namna ya kuandaana ili kuondoa hatari ya kupata michubuko ambayo inaweza kupelekea kupata maambukizi.

 

Mwathirika kutumia dawa ipasavyo

 

Mwathirika wa VVU anatakiwa kutumia dawa za kudhoofisha maambukizi ya VVU ipasavyo ili kusaidia kushusha kiwango cha virusi kwenye damu. Endapo mwathirika atazigatia matumizi ya dawa ipasavyo, kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana kiasi kwamba kutoweza kuonekana kwenye damu kirahisi.  Kipindi ambacho mwathirika wa VVU ana kopi ya virusi ambao hawasomeki kwenye damu huwa ni salama sana kwani ni vigumu kuambukiza virusi kwa mtu mwingine. Soma Zaidi kuhusu namna gani virusi hushuka chini katika Makala zingine ndani ya tovuti hii. Ili kuweza kufikia malengo ya kushusha nakala za virusi vya UKIMWI kwenye damu kwenda katika kiwango ambacho hakitambuliki kwenye damu au chini ya nakala 50 kwa microlita moja, unapswa kutumia dawa zako kila siku bila kukosa na pia kuhudhuria kwenye kliniki yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

 

Wakati wa kutafuta mtoto jiandaeni vema

 

Wakati wa kutafuta watoto ni lazima mjiandae vema haswa katika tendo, unashauriwa kutafuta mtoto katika kipindi ambacho

 

Je mahusiano ya mpenzi mmoja mwenye VVU na asiye navyo yapo?

 

Ndio mahusiano yapo mengi sana kati ya mwathirika wa VVU na mtu ambaye hana virusi vya ukimwi

 

Je ninaweza kutoambukizwa VVU endapo nitakuwa na mpenzi mwenye VVU?

 

Ndio inawezekana usipate maambukizi endapo unashiriki ngono na mpenzi mwenye VVU. Hii itakuwa kweli endapo unazingatia ushauri wa daktari wako wa namna ya kuishi na mwathirika wa VVU. Makala ya namna ya kujamiana na mwathirika pasipo kupata maambukizi ya VVU imeelezea vema kwa jinsi gani unaweza kujamiana na mwathirika pasipo kupata maambukizi. Bonyeza hapa kuisoma Zaidi.

 

Je wapenzi wenye mahusiano haya huweza kupata watoto bila kuwaambukiza?

 

Ndio inawezekana wapenzi ambao wapo kwenye mahusiano na hali yao mmoja hajaambukizwa VVU kupata mtoto ambaye hana maambukizi endapo watafuata ushauri wa kitaalamu kuzuia maambukizi kwa mtoto.

 

​​

Imeboreshwa 10.01.2021

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile mara baada ya kusoma makala hii.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' Chini ya tovuti hii.

​

​

  1. Tewodros G Hailemariam etal.  Sexual life and fertility desire in long-term HIV serodiscordant couples in Addis Ababa, Ethiopia: a grounded theory study. https://bmcpublichealth.biomedcentral.com/articles/10.1186/1471-2458-12-900. Imechukuliwa 10.01.2021

  2. R. E. Bunnell ScD Med etal. Living with discordance: knowledge, challenges, and prevention strategies of HIV-discordant couples in Uganda. https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1080/09540120500100718?scroll=top&needAccess=true&journalCode=caic20. Imechukuliwa 10.01.2021

  3. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3778788/. Imechukuliwa 10.01.2021

bottom of page