top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Jamiana na mwenye VVU pasipo kupata maambukizi| ULY CLINIC

Je inawezekana kutopata VVU ukijamiana na mwathirika wa VVU pasipo kinga?


Je sababu gani zinasababisha mtu asipate maambukizi hata baada ya kujamiana na mwathirika wa VVU?



Maswali haya yamekuwa yakiulizwa sana na watu kupitia kwenye barua pepe ya tovuti hii, naam hata wewe inawezekana ulishawahi kutana na swali hili au mazingira kama haya. Katika makala hii utajifunza kitu kuhusu majibu ya maswali haya kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika

VVU huambukizwaje?

Kuna njia mbalimbali za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI zinazofahamika, njia hizo zimeorodheshwa kwenye makala mbalimbali ndani ya tovuti hii (Bonyeza hapa kusoma kuhusu maambukizi ya VVU) lakini katika makala hii imejikita kujibu maswali ya njia moja kuu ya maambukizi ambayo ni njia ya kujamiiana UKE kwa UUME.


Ili kuweza kujibu maswali yaliyoulizwa ni vema kupitia vidokezo mbalimbali kuhusu maambukizi kwa njia hii.

  • Unaweza jamiana na mwathirika wa VVU pasipo kupata maambukizi ya VVU bila hata kutumia kinga

  • Ukijamiana na mwathirika wa VVU anayetumia dawa za ARV unakuwa kwenye bahati kubwa ya kutoambukizwa VVU

  • Endapo una magonjwa ya zinaa, ukijamiana na mwathirika wa VVU unakuwa na hatari kubwa ya kupata VVU kuliko ukiwa huna magonjwa hayo

  • Mwathirika wa VVU endapo ana magonjwa mengine nyemelezi au akiwa kwenye hatua ya mwisho ya VVU yaani UKIMWI ana hatari kubwa ya kuambukiza wengine endapo atajamiana pasipo kinga

  • Michubuko kwenye sehemu za siri inaongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU endapo utashiriki bila kinga

  • Kuandaliwa vema kwa mwanamke kunapunguza uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamiana na kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya VVU

  • Mwanamke asiye na VVU akishiriki na mwanaume mwenye VVU ana hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya VVU kuliko kinyume chake

Kwanini sijapata Maambukizi ya VVU licha ya kushiriki na mwathirika wa VVU

Hatari ya kupata au kutopata maambukizi hutegemea hali ya kinga za mwili za mwathirika na kiwango cha virusi kwenye damu ambacho hupimwa kwa kipimo kinachoitwa viral load. Maelezo ya hapa chini yanaonyesha uwezekano wa kupata au kutopata maambukizi kwa kujamiana UKE kwa UUME tu na mwathirika wa VVU pasipo kutumia kinga


Kujamiana kwa mwanamke mwenye maambukizi na mwanaume asiye na maambukizi

  • Uwezekano wa mwanaume kutopata VVU ni asilimia 99.99957 ( kwa maana nyingine inatakiwa ujamiane na mwanamke huyo mara 2380 ili kuweza kupata maambukizi kutoka kwake)

Kujamiana kwa mwanamke mwenye maambukizi na mwanaume asiye na maambukizi huku kipimo cha viral load kuonyesha virusi havipo kwenye damu

  • Uwezekano wa mwanaume kutopata VVU ni asilimia 100

Kujamiana kwa mwanaume mwenye maambukizi na mwanamke asiye na maambukizi

  • Uwezekano wa mwanamke kutopata VVU ni asilimia 99.999189 ( kwa maana nyingine inatakiwa ujamiane na mwanaume huyo mara 1234 ili kuweza kupata maambukizi kutoka kwake)

Kujamiana kwa mwanaume mwenye maambukizi na mwanamke asiye na maambukizi huku kipimo cha viral load kuonyesha virusi havipo kwenye damu

  • Uwezekano wa mwanamke kutopata VVU ni asilimia 100


Ni nini kinasababisha kutopata maambukizi ya VVU licha ya kushiriki na mwathirika?

Sababu kuu zinazopelekea kutopata maambukizi ya VVU licha ya kushiriki na mwathirika wa VVU zimeelezewahapa chini;


Idadi ya virusi kwenye damu


Kiwango cha virusi vya UKIMWI kwenye damu huwa kikubwa pale mwathirika akiwa kwenye hatua ya awali ya maambukizi, kipindi hiki ni kile cha ndani ya mwezi mmoja wa kupata maambukizi ambapo mwathirika huonyesha dalili za awali kabisa za kuambukizwa VVU(bonyeza hapa kusoma zaidi)


Hata hivyo kwenye hatua za mwisho za VVU ambapo mgonjwa anaonyesha dalili za UKIMWI(magonjwa nyemelezi), kiwango cha virusi kwenye damu huwa kikubwa sana.

Kipindi hiki hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine na huchukua takribani miaka miwili hadi 10 kwa mtu kuanza kuonyesha dalili za UKIMWI.

Mwathirika w VVU anayetumia dawa za ARV kwa usahihi, huweza kupunguza kiwango cha VVU kwenye damu na kufikia wakati ambapo virusi havionekani kabisa kwenye damu. Kipindi hiki mwathirika huyu huwa hana uwezo kabisa wa kuambukiza mtu mwingine kwa njia ya kujamiana uke kwa uume.

Kwa muhitasari, kiwango kikubwa cha virusi kweye damu huongeza hatari mara sita hadi saba zaidi ya kuambukiza mtu mwingine VVU

Kuwa na magonjwa ya zinaa


Endapo mtu hana VVU lakini ana magonjwa ya zinaa kama kaswende au gono, anakuwa kwenye hatari mara mbili zaidi kupata maambukizi ya VVU endapo atashiriki na mtu aliyeambukizwa bila kutumia kondomu

Unaweza uliza maswali zaidi na ukajibiwa na daktari wa ULY CLINIC

ULY CLINIC inakushauri, wasiliana na mtaalamu wa afya kabla ya kuchukua hatua yoyote ile mara baada ya kusoam makala hii.

Soma makala zingine kuhusu hatari ya kupata maambukizi kwa njia zingine za kujamiana mbali na uke kwa uume katika tovuti yetu.

Rejea za mada;


  1. NAM AIDSmap. Estimated HIV risk per exposure. https://www.aidsmap.com/about-hiv/estimated-hiv-risk-exposure. Imechukuliwa 09.11.2020

  2. AIDS. Risk of HIV-1 transmission for parenteral exposure and blood transfusion: a systematic review and meta-analysis. https://journals.lww.com/aidsonline/Fulltext/2006/04040/Risk_of_HIV_1_transmission_for_parenteral_exposure.3.aspx. Imechukuliwa 09.11.2020

  3. JAMA. Sexual Activity Without Condoms and Risk of HIV Transmission in Serodifferent Couples When the HIV-Positive Partner Is Using Suppressive Antiretroviral Therapy. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/2533066. Imechukuliwa 09.11.2020

  4. ULY CLINIC. Dalili za UKIMWI. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ukimwi.Imechukuliwa 09.11.2020

  5. ULY CLINIC. Maambukizi ya VVU. https://www.ulyclinic.com/ukimwi. Imechukuliwa 09.11.2020

  6. AIDS catie. Putting a number on it: The risk from an exposure to HIV. https://www.catie.ca/en/pif/summer-2012/putting-number-it-risk-exposure-hiv. Imechukuliwa 09.11.2020

1,166 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page