top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

9 Oktoba 2021 08:26:10

Barakoa, miwani na COVID-19

Kama COVID-19 inaingia kupitia macho, pua na mdomo kwanini tunasisitizwa kuvaa barakoa bila kuvaa miwani?

Corona huenea pale majimaji kutoka kwenye njia ya hewa ya mtu mwenye maambukizi yanapoingia mwilini kupitia puani, mdomoni au machoni. Uvaaji wa barakoa husaidia kuzuia majimaji yanayotoka kwenye njia ya hewa yasisambae na kuwaathiri wengine pale mtu anapopiga chafya au kukohoa au kupenga makamasi. Vile vile hakikisha unanawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au safisha mikono kwa kutumia kitakasa mikono (sanitizer), na pia epuka kugusa maeneo ya usoni kwa mikono ambayo haijasafishwa ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 09:16:21

Rejea za mada hii

bottom of page