top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021 10:49:24

Barakoa na kunawa mikono hukinga kirusi kipya cha COVID-19?

Je kunawa mikono na kuvaa barakoa kunasaidia kujikinga dhidi ya kirusi kipya cha COVID-19?

Ndio!

Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni husaidia kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kuenea kupitia mikono michafu ikiwemo COVID-19. Pia uvaaji wa barakoa husaidia kujinga na kumkinga mwingine dhidi ya magonjwa yatokana na majimaji ya yatokayo mdomoni na puani (ikiwemo COVID-19) ili kuzuia majimaji hayo yasisambae kwa wengine au yasikufikie wewe pale wewe na mtu mwingine anapokohoa, kupiga chafya au kuongea. Hivyo unashauriwa kuhakikisha unafuata kanuni za afya ili kujikinga na haya magonjwa.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 12:28:04

Rejea za mada hii

bottom of page