Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
9 Oktoba 2021 08:50:14
Kwanini kila nchi yenye uwezo inatengeneza chanjo yake ya Corona? Zina utofauti gani? Ipi ni bora na sahihi?
Chanjo kama zilivyo dawa nyingine hutengenezwa na makampuni tofauti na zote hupewa majina (brand name) kulingana na kampuni iliyotengeneza. Chanjo hizi hazina utofauti wa ubora wa kazi inayofanywa na chanjo hiyo hivyo zote ni salama na zina ufanisi wa hali ya juu katika kuzuia maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, kuzuia ugonjwa mkali wa COVID-19, na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021 09:14:19
Rejea za mada hii
https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019/question-and-answers-hub. Imechukuliwa 09.10/2021