top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

10 Oktoba 2021 15:35:27

Chanjo kwa  wenye kinga ya chini na wazee

Mzee na watu wenye magonjwa tunasema kinga zao ziko chini sana kwanini wanapewa chanjo na inafanyaje kazi?Kama kiasili miili yao haina kinga?

Watu wenye kinga ya chini pamoja na wazee wanapewa chanjo ili miili yao iweze kutengeneza kinga mapema kabla hawajaambukizwa. Pamoja na kwamba kinga ya mwili inapungua kidogo kwa wazee wenye umri mkubwa lakini haipotei kabisa na bado wanao uwezo wa kutengeneza kinga. Kwa hiyo inashauriwa wapewe chanjo haraka na mapema kama inawezekana.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

10 Oktoba 2021 15:35:27

Rejea za mada hii

bottom of page