top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

9 Oktoba 2021 07:42:01

Chanjo ya COVID-19 iwekwe kwenye Pentavalent

Kwanini chanjo ya Corona isiunganishwe kwenye pentavalent ili Watoto wapate kinga wakiwa bado wadogo kwa inavyoonekana hili janga la Corona haliishi leo wala kesho?

Matumizi ya chanjo huongozwa na matokeo ya tafiti za kisayansi. Tafiti za awali zilifanyika kwa watu wazima, ndio maana chanjo kwa sasa wanapewa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18. Lakini tafiti za matumizi ya chanjo kwa watoto zimeanza na zinaendelea. Zitakapokamilika zitatupa muongozo wa jinsi ya kutumia chanjo hizi kwa watoto wadogo. Hata hivyo, hadi sasa, watoto si kundi linaloathirika sana na COVID-19.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 09:16:31

Rejea za mada hii

bottom of page