Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 10:42:17
Je kirusi kipya cha COVID-19 kina chanjo?
Kirusi tunachopambana nacho kwa sasa siyo kirusi kipya, bali ni anuai mpya ya kirusi kile kile cha Corona ila kinajibadilisha badilisha, ambayo ni tabia ya virusi karibia vyote ili viweze kimejibadilisha zaidi.
Mabadiliko haya yamefanya anuai hii ya kirusi kuweza kusambaa zaidi. Bahati nzuri, chanjo ambazo zipo mpaka sasa hivi pia zinasaidia kumpa mtu kinga dhidi ya hii anuwai mpya ya kirusi cha Corona.Hata hivyo inawezekana ufanisi wa hizi chanjo usiwe wa kiwango kile cha anuwai za awali, lakini bado chanjo hizi zinatoa kinga kwa kiwango kinachokubalika kimataifa dhidi ya hii anuwai mpya na kuzuia ugonjwa mkali, kulazwa na vifo.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 12:28:07
Rejea za mada hii