Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 10:29:59
Je, kuna dalili mpya za kirusi cha COVID-19?
Wigo wa dalili za COVID-19 umekuwa ukipanuka tangu tulivyopata wimbi la kwanza na mpaka sasa kwenye
wimbi ili la tatu.
Dalili za awali kabisa wakati wa wimbi la kwanza zilikuwa ni pamoja
Kikohozi kikavu
Koo kukereketa/kuwasha
Homa
Kubanwa na kifua/mbavu
Mwili kuchoka
Maumivu ya kichwa
Baadaye zikaongezeka dalili nyingine kama vile;
Kutohisi harufu
Kutohisi ladha
Macho mekundu
Vipele
Kukosa hamu ya kula
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 12:28:08
Rejea za mada hii