Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
10 Oktoba 2021, 13:27:40
Je, chanjo ya China inatumika Tanzania?
Kwa sasa chanjo inayotolewa Tanzania bara ni J&J (Janssen). Chanjo mojawapo inayotumika Zanzibar in Sinovac iliyotengenezwa China. Hata hivyo, chanjo yeyote iliyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani kuhakikiwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) zinaweza kutumika, ambazo ni Pfizer, Moderna, Janssen, Sinovac na Sinopharm. Orodha hii ya chanjo zilizopendekezwa inaweza kubadilika muda wowote ule kulingana na ushahidi wa kisayansi kadri unavyopitiwa na Kamati ya Kitaalamu
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
10 Oktoba 2021, 13:27:40
Rejea za mada hii