top of page

Mwandishi:

Dkt. Lugonda B, MD

Mhariri:

Dkt. Wambura C, MD

14 Novemba 2021 19:06:35

Je, kuna madhara gani ya bakteria vajinosis kwa mjamzito?

Je, kuna madhara gani ya bakteria vajinosis kwa mjamzito?

Bakteria vajinosis (BV) hufahamika kusababisha kutokwa na uchafu ukeni kwa wanawake walio katika umri wa kubeba mimba. BV husababishwa na mchanganyiko wa maambukizi ya vimelea unaoamshwa na kubadilika kwa mazingira ya uke baada ya kupoteza vimelea wake asili.


Je Bakteria vajinosisi ni ugonjwa wa zinaa?


Hapana!


Hata hivyo icha ya bakteria vajinosis kutochukuliwa kuwa ugonjwa wa zinaa, umekuwa ukihusianishwa na kujamiana.


Dalili za vajinosis ya bakteria


Wajawazito (na wasio wajawazito) wenye Bakteria Vajinosis wanaweza wasionyeshe dalili au wakawa na dalili zifuatazo;


  • Kutokwa na uchafu ukeni

  • Kutokwa na uchafu wenye harufu ya uozo

  • Kutokwa na harufu ya samaki ukeni


Madhara gani ya bakteria vajinosis kwa mjamzito


Bakteria vajinosis kwa mjamzito huweza ambatana na madhara makubwa kama vile;


  • Kupasuka kwa chupa ya uzazi

  • Uchungu kabla ya wakati

  • Kujifugua kabla ya wakati

  • Maambukizi ya vimelea kwenye chupa ya uzazi

  • Endometraitis


Uchunguzi


Ingawa hakuna ushahidi wa kupima wanawake wajawazito bakteria vajinosis, wajawazito wenye dalili wanapaswa kuchunguzwa na kupata matibabu.


Je kuna madhara ya moja kwa moja kwa mtoto ya bakteria vajinosis?


Hakuna madhara ya moja kwa moja yanayofahamika kutokea kwa mtoto. Madhara mengi yanayotokea huhusiana na madhara anayopata mama na hivyo kupelekea madhara yasiyo ya moja kwa moja. Mfano kama chupa ya uzazi itapasuka mapema, mama atapata mtoto njiti n.k.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

14 Novemba 2021 19:14:54

Rejea za mada hii

  1. Nelson DB, et al. Bacterial vaginosis in pregnancy: current findings and future directions. Epidemiolo Rev 2002;24(2):102–8.

  2. Hauth JC, etal. Reduced incidence of preterm delivery with metronidazole and erythromycin in women with bacterial vaginosis. N Engl J Med 1995;333:1732–6.

  3. McDonald HM, et al. Impact of metronidazole therapy on preterm birth in women with bacterial vaginosis flora (Gardnerella vaginalis): a randomized, placebo controlled trial. Br J Obstet Gynecol 1997;104:1391–7.

  4. Morales WJ, et al. Effect of metronidazole in patients with preterm birth in preceding pregnancy and bacterial vaginosis: a placebo-controlled, double blind study. Am J Obstet Gynecol 1994;171:345–9.

bottom of page