Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
14 Novemba 2021 10:25:54
Je, kuna madhara gani ya chlamydia kwa mjamzito?
Chlamydia ni ugonjwa maarufu wa zinaa unaoambukizwa kwa njia ya kujamiana na unaosababishwa na bakteria.
Dalili
Licha ya wanawake wenye chlamydia kutoonyesha dalili mara nyingi, maambukizi hayo huweza jionyesha kwa dalili zifuatazo;
Kutokwa na uchafu usioeleweka ukeni
Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiana
Hisia za kuungua au kuwashwa kwenye njia ya mkojo wakati wa kukojoa
Madhara
Kama maradhi ya chlamydial yasipotibiwa kwa wakati hupelekea mama mjamzito kupata madhara yafuatayo;
Uchungu kabla ya wakati
Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati
Kujifungua mtoto njiti
Kujifungua mtoto mwenye uzito kidogo
Madhara kwa kichanga
Mtoto anapokuwa anapita kwenye tundu la uzazi huweza pata maambukizi yanayoweza pelekea magonjwa ya macho na mapafu.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
14 Novemba 2021 10:28:26
Rejea za mada hii
Andrews WW, et al. The Preterm Prediction Study: association of second-trimester genitourinary Chlamydia infection with subsequent spontaneous preterm birth. Am J Obstet Gynecolo 2000;183;662–8.
Alger LS, et al. The association of Chlamydia trachomatis, Neisseira gonorrhoeae, and group B streptococci with preterm rupture of the membranes and pregnancy outcome. Am J Obstet Gynecol 1988;159(2):397–404.