top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Peter A, MD

21 Novemba 2021 08:54:04

Je, ngozi kuwasha ni dalili ya VVU?

Je, ngozi kuwasha ni dalili ya VVU?

Jibu ni Ndio au Hapana. Hii ni kwa sababu harara kwenye ngozi inayoambatana na muwasho, maumivu, ngozi kubadilika rangi, malenge huweza kutokea kwa mtu yeyote awe na maambukizi au la licha ya kutokea sana kwa waathirika wa VVU.


Muwasho kwa waathirika wa VVU huweza kusababishwa na;


  • Mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya VVU

  • Kushuka kwa kinga mwilini

  • Magonjwa nyemelezi

  • Mwitikio wa kinga ya mwili kwenye dawa za ARV

  • Saratani

  • Magonjwa mengine


Soma zaidi kuhusu harara za VVU, muwasho wa ngozi na matibabu yake kwenye makala zingine za ULY CLINIC

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

21 Novemba 2021 09:19:45

Rejea za mada hii

  1. Roland M. Itchy skin in HIV. Newsline People AIDS Coalit N Y. 1998 Mar:21-5. PMID: 11367452.

  2. Altman, et al. “Cutaneous manifestations of human immunodeficiency virus: a clinical update.” Current infectious disease reports vol. 17,3 (2015): 464. doi:10.1007/s11908-015-0464-y

bottom of page