Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
14 Novemba 2021, 08:22:42
Madhara ya gono kwa mjamzito
Gono ni jina linalotumika na watu wengi lililotokana na ugonjwa gonorrheal na huwa na maana pia ya kisonono. Ugonjwa huu husabaishwa na bakteria mwenye jina la Neisseria gonorrhea ambaye huenezwa kwa kujamiana na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga.
Madhara kwa mama mjamzito
Yapo madhara kadha wa kadhayanayoweza kutokea wakati wa ujauzito kama mama mjamzito asipopata matibabu ya gono ambayo ni;
Mtoto kuzaliwa akiwa na upofu
Kuharibika kwa mimba
Kujifungua njiti
Kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati
Maambukizi kwenye chupa ya uzazi
Kusoma zaidi kuhusu gono, vihatarishi na madhara kwa ujumla ingia kwenye makala ya gono.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
14 Novemba 2021, 19:18:49
Rejea za mada hii
CDC. S.T.I in pregnancy. https://www.cdc.gov/std/pregnancy/stdfact-pregnancy-detailed.htm. Imechukuliwa 14.11.2021