Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
13 Novemba 2021, 16:33:45
Madhara ya kutopata tiba ya usaha sehemu za siri
Madhara ya kutopata matibabu maradhi ya kutokwa na usaha sehemu za siri kwa mwauame na mwanamke yameelezewa katika makala hii;
Madhara kwa mwanamke
Kutopata matibabu kwa wakati kwa mwanamke na mwanaume anayetokwa na usaha sehemu za siri hupelekea kupata matatizo ya kudumu kama maambukizi ya PID yanayapolekea;
Kutengenezwa kwa makovu kwenye mirija ya uzazi yanayosababisha kuziba kwa mirija ya uzazi
Mimba kutungwa nje ya kizazi
Ugumba
Maumivu ya kudumu ya via ndani ya nyonga na tumbo
Madhara kwa mama mjamzito
Madhara ya gono kwa mama mjamzito na mtoto tumboni ni pamoja na;
Upofu kwa mtoto
Mimba kutoka
Kujifungua njiti
Kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati
Maambukizi kwenye chupa ya uzazi
Madhara kwa mwanaume
Madhara kwa wanaume ni;
Maumivu sugu kwenye njia ya mkojo na korodani
Makovu kwenye mrija urethra
Ugumba
Kusambaa kwa vimelea kwenye damu( ni kwa nadra sana na kama ikitokea hutishia maisha)
Madhara mengine
Huongeza hatari ya kupata magonjwa mengine ya zinaa kama UKIMWI
Nini unapaswa kufahamu zaidi?
Makala hii imejibu kuhusu;
Kuhusu madhara ya usaha sehemu za siri
Madhara ya kutopata matibabu ya usaha sehemu za siri kwa wakati
Madhara ya kutopatamatibau ya gono
Madhara ya Chlamydia trachomatis
Madhara ya Neisseria gonorrhoeae
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
14 Novemba 2021, 10:00:47
Rejea za mada hii
Centers for Disease Control and Prevention. Gonorrhea. CDC fact sheet (detailed version). https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea.htm. Imechukuliwa 13.11.2021
Ghanem KG. Clinical manifestations and diagnosis of Neisseria gonorrhoeae infection in adults and adolescents. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 13.11.2021
Gonorrhea CDC Fact Sheet. https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea.htm. Imechukuliwa 13.11.2021
Chapter 3. Urethral Discharge. https://accessmedicine.mhmedical.com/content.aspx?bookid=369§ionid=39914779. Imechukuliwa 13.11.2021
Merck Manual Professional Version. Gonorrhea. https://www.merckmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea. Imechukuliwa 13.11.2021
Office on Women's Health. Gonorrhea. https://www.womenshealth.gov/a-z-topics/gonorrhea. Imechukuliwa 13.11.2021
Speer ME. Gonococcal infection in the newborn. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 13.11.2021
CDC. STI in pregnancy. https://www.cdc.gov/std/pregnancy/stdfact-pregnancy-detailed.htm#. Imechukuliwa 13.11.2021