top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

ULY CLINIC

12 Agosti 2023, 17:25:41

Je, PID inatibika?

Je, PID inatibika?

Ndio

PID inaweza kutibika na kuisha kabisa (kuponyeka) endapo itagunduliwa mapema na kutibiwa kwa dawa sahihi. Hata hivyo matibabu hayaondoi madhara na uharibifu wowote uliokwisha tokea kwenye mfumo wa uzazi kutokana na ugonjwa.


Jinsi unavyochelewa kupata matibabu unaongeza uwezekano wa kupata uharibifu mkubwa kwenye via vya uzazi unaoweza kupoteza uwezo wako wa kushika mimba au ugumba.


Mambo muhimu ya kufahamu pia

  • Unapotumia dawa hakikisha kuwa unamaliza dozi, hii ni kwa sababu unapoanza dawa daili hupotea na hivyo watu wengi huacha kumaliza dozi na ugonjwa huendelea.

  • Hakikisha mpenzi wako wa hivi karibuni unayeshiriki naye ngono anapima na kupata matibabu ya magonjwa ya zinaa kabla ya kushiriki ngono aina yoyote ile ili kuhakikisha kuwa hamuambukizani upya.

  • Unaweza kupata PID kwa mara nyingine kama ukiambukizwa na magonjwa ya zinaa. Na kama umeshawahi kupata PID, una hatari kubwa ya kupata PID kwa mara nyingine.


Wapi unapata maelezo ya ziada?

Pata maelezo ya ziada katika makala zingine zinazohusu PID kwa kubofya linki zinazofuata

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Agosti 2023, 18:19:08

Rejea za mada hii

  1. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Pelvic Inflammatory Disease. ACOG Patient Education Pamphlet, 1999.

  2. Westrom L and Eschenbach D. In: K. Holmes, P. Sparling, P. Mardh et al (eds). Sexually Transmitted Diseases, 3rd Edition. New York: McGraw-Hill, 1999, 783-809.

bottom of page