top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

7 Novemba 2021 09:57:18

Je, unajuaje p2 imefanya kazi?

Je, unajuaje p2 imefanya kazi?

Kufahamu kama p2 imefanyaka kazi au la ni swali ambalo limeulizwa sana na watumiaji wa P2. Katika makala hii imeelezea njia mbalimbali za kufahamu kama dawa hii imefanya kazi au la.


Njia za kutambua

NJia zifuatazo huashiria kuwa p2 imefanya kazi;


Kuingia hedhi

Utafahamu kuwa p2 imefanya kazi kama utapata period inayofuata na ni inaonekana kuwa ya kawaida. Kwa kawaida utaingia kwenye piriodi yako ndani wiki 2 hadi 3 zinazohesabiwa kutoka kwenye siku yako ya hatari. kwa wanawake ambao mzunguko wao wa hedhi ni ziku 28, huona periodi ndani ya siku 12 hadi 16 tangu kuingia kwenye siku ya hatari.


Kupima ujauzito

Kama P2 imefanya kazi, baada ya wiki mbili tangu siku yako ya hatari, kipimo cha ujauzito kinachotumia mkojo kitaonyesha hauna ujauzito. Na kama umepata ujauzito kipimo hicho kitachora mstari unaoashiria kuwa una ujauzito. Unaweza kuthibitisha pia kwa kutumia kipimo cha Ultrosound.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

6 Agosti 2023 08:01:06

Rejea za mada hii

bottom of page