Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
8 Novemba 2021, 06:07:00
Je, vipimo vya tezi dume ni vipi?
Makala hii imetumia neno vipimo vya tezi dume iliyovimba au vipimo vya kuvimba tezi prostate kumaanisha vipimo vya tezi dume
Tezi dume iliyokuwa
Kukua kwa tezi dume, ni tendo endelevu lisilo saratani linalohusisha ongezeka la umbile au ujazo wa tezi dume (prostate). Prostate ni tezi ndogo (yenye ujauzo wa gramu 25) inayozunguka mrija wa urethra kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume. Huwa na kazi ya kuzalisha majimaji yenye virutubisho vya kulisha na kusafirisha manii.
Dalili za tezi dume iliyokuwa
Dalili za prostate iliyokuwa ni;
Hisia za mkojo kubakia ndnai ya kibofu hata baada ya kukojoa wote
Kukojoa mara kwa mara
Kukatishwa na kuanza kwa mkondo wa mkojo wakati wa kukojoa
Kushindwa kuzuia mkojo
Mkondo dhaifu wa mkojo
Kutumia nguvu wakati wa kutoa mkojo
Kukojoa sana wakati wa usiku
Vihatarishi
Kukua kwa tezi dume hutokea sana kwa;
Wanaume wenye zaidi ya miaka 40
Wenye historia ya kuvimba tezi dume ( baba au kaka)
Wenye asili ya Afrika na waafrika wa Amerika ( hupata kwenye umri mdogo ukilingnaisha na watu wenye asili ya Asia)
Wenye historia ya magonjwa sugu kama obeziti, kisukari aina ya 2 na magonjwa ya moyo
Wasioshughulisha mwili
Wenye madhaifu ya kusimamisha uume
Vipimo vya kufanya
Vipimo ambavyo hutumika kudhibitisha tezi dume iliyokuwa baada ya kuwa na dalili hizo na vihatarishi ni;
Vipimo vya maabara
Prostate specific antigen (PSA) huongezeka kwa wanaume wenye saratani ya tezi dume pia hata waliovimba tezi dume
Uchunguzi wa mkojo- ili kuangalia dalili za maambukizi ya U.T.I au damu kwenye mkojo
Kipimo cha kuotesha mkojo- huangalia uwepo wa vimelea vya U.T.I kwenye mkojo
Kiwango cha madini, yurea na nitrojeni kwenye damu (BUN) na kiwango cha creatinine – hutumika kuangalia utendaji kazi wa figo
Vipimo vingine
Kipimo cha kuchunguza tezi dume kwa vidole vya mtaalamu- hulenga kugundua umbile na ukubwa wa tezi
Ultrasound ya tezi dume – hutumika kuchunguza ujazo wa tezi dume, kuangalia uwezo wa kibofu kutunza mkojo.
Sistoscopi – huchunguza mrija wa urethra na kibofu cha mkojoa
Kipimo cha uwezo wa mkojo kutoka na shinikizo la mkojo- hulenga kupima uwezo wa mkojo kupita kwenye mrija wa urethra na kiwango cha shinikizo la ndnai ya kibofu cha mkojo wakati w akukojoa.
Kukata kinyama kwenye tezi dume – hutumia kinywama kidogo kutoka kwenye tezi dume ili kwenda kufanyiwa uchunguzi wa mwonekano wa chembe hai za tezi dume kama ni za kawaida au zimekuwa na sifa ya saratani.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Februari 2022, 04:51:38
Rejea za mada hii
Barry MJ, et al. The American Urological Association Symptom Index for Benign Prostatic Hyperplasia. The Journal of Urology. 2017; 197: S189-S197. DOI: http://dx.doi.org/10.1016/j.juro.2016.10.071 American Urological Association. Management of Benign Prostatic Hyperplasia. https://www.auanet.org/guidelines/benign-prostatic-hyperplasia-(2010-reviewed-and-validity-confirmed-2014). Imechukuliwa 8/11/2021
Cooperberg MR, et al. Chapter 23. Neoplasms of the Prostate Gland. In: McAninch JW, Lue TF. eds. Smith and Tanagho’s General Urology, 18e New York, NY: McGraw-Hill; 2013.
Deters LA. (6 Nov 2016 updated.) Benign Prostatic Hypertrophy. Available online at http://emedicine.medscape.com/article/437359-overview?pa=pjcpJFziVtidyc3mPZw0nI0kS%2BN6TaVIM%2FiDWCbEIpwI33GP4LRnoLbt2MSIkCyikMxRGSC7BjbG0fgXxUgsJXf7Bj2Gvk6BKC47oRZ1BB8%3D#a7. Imechukuliwa 8/11/2021
Mayo Clinic. (13 Nov. 2014 updated.) Benign Prostatic Hyperplasia (BPH). http://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/benign-prostatic-hyperplasia/basics/definition/con-20030812. Imechukuliwa 8/11/2021
Miteshkumar RT et al. Digital rectal examination, transrectal ultrasound, and prostate specific antigen as triple assessment diagnostic tool for benign enlargement of prostate. Natl J Med Research 2015; 5(3):244-248.
National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. (Sept 2014 updated.) Prostate Enlargement (Benign Prostatic Hyperplasia). https://www.niddk.nih.gov/health-information/urologic-diseases/prostate-problems/prostate-enlargement-benign-prostatic-hyperplasia. Imechukuliwa 8/11/2021
Scher HI, et al. Benign and Malignant Diseases of the Prostate. In: Kasper D, Fauci A, Hauser S, Longo D, Jameson J, Loscalzo J. eds. Harrison’s Principles of Internal Medicine, 19e New York, NY: McGraw-Hill; 2014.
Urology Care Foundation. Benign Prostatic Hyperplasia (BPH). http://www.urologyhealth.org/urologic-conditions/benign-prostatic-hyperplasia-(bph). Imechukuliwa 8/11/2021