top of page

Mwandishi:

Dkt. Lusenge S, MD

Mhariri:

Dkt. Sospeter M, MD

8 Julai 2023 19:51:15

Je kuna madhara yoyote ya kutumia PEP kwa muda mrefu?

Je, kuna madhara ya kutumia PEP muda mrefu?

PEP ni kifupisho cha neno la kitaalamu Post Exposure Prophylaxis lenye maana ya matumimizi ya ARV kwa mtu ambaye amekuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.


Hakuna madhara yoyote ya kutumia PEP kwa muda mrefu endapo mtumiaji hana matatizo ya ini na figo. Isipokuwa mtumiaji anaweza kupata maudhi ya ARV ambayo huisha ndani ya muda mfupi kama vile;

  • Mwili kuchoka

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kichwa kuuma

  • Kukosa usingizi

Nini unapaswa kufahamu zaidi?

Lengo la PEP ni kumlinda mtu baada ya kuwa katika hatari ya kupata mambukizi ya VVU katika mazingira yasiyoweza epukika.

PEP haipaswi kutumika kama kinga dhidi ya VVU hivyo basi marazote unapaswa kutumia njia nyingine za kujilinda na VVU kama kutumia kondomu, kutoshiriki ngono isiyo salama nk.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

8 Julai 2023 19:59:08

Rejea za mada hii

  1. How Do I Prescribe PEP? | Prevention | Clinicians | HIV | CDC.https://www.cdc.gov/hiv/clinicians/prevention/prescribe-pep.html. Imechukuliwa 06.07.2023

  2. About PEP - HIV Basics - Centers for Disease Control and Preventionhttps://www.cdc.gov/hiv/basics/pep/about-pep.html. Imechukuliwa 06.07.2023

  3.  Post-Exposure Prophylaxis (PEP): Definition, Side Effects, and Medications. webmd.com.https://www.webmd.com/hiv-aids/post-exposure-prophylaxis.Imechukuliwa 06.07.2023

bottom of page