top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

12 Oktoba 2021 19:16:18

Je ni muda gani mzuri wa kumeza amlodipine?

Je ni muda gani mzuri wa kumeza amlodipine?

Haijalishi ni muda gani utameza amlodipine iwe asubuhi, jioni au usiku. Jambo la msingi ni kumeza muda unaotakiwa kama uliyopangiwa na daktari wako ilikuongeza ufanisi wa dawa.


Amlodipine ni dawa jamii kifunga njia ya kalisiamu, inayofanya kazi kwa kuongeza kipenyo cha mishipa ya damu ili kupunguza shinikizo la juu la damu. Hata hivyo hutumika pia kutibu maumivu ya kifua kutokana na anjaina na magonjwa mengine kutokana na magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo.


Unaeza kutumia amlodipine pia pamoja au pasipo chakula kwa kuwa chakula hakina mwingilinao na ufyonzwaji wa dawa, hata hivyo unapaswa kuepuka vyakula kama;


  • Zabibu au juisi ya zabibu

  • Licorice asilia

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Oktoba 2021 19:16:18

Rejea za mada hii

  1. Drugbank. Amlodipine. https://go.drugbank.com/drugs/DB00381. Iemchukuliwa 11.10.2021

  2. van Zwieten PA: Amlodipine: an overview of its pharmacodynamic and pharmacokinetic properties. Clin Cardiol. 1994 Sep;17(9 Suppl 3):III3-6

  3. Fares H, et al. Amlodipine in hypertension: a first-line agent with efficacy for improving blood pressure and patient outcomes. Open Heart. 2016 Sep 28;3(2):e000473. doi: 10.1136/openhrt-2016-000473. eCollection 2016.

bottom of page