top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

ULY CLINIC

Imeboreshwa:

4 Februari 2026, 04:08:42

Kikokotoo: Kipimo cha mimba kwa mkojo baada ya Mimba kutoka

Kikokotoo: Kipimo cha mimba kwa mkojo baada ya Mimba kutoka

Kikokotoo hiki kimeandaliwa ili kukupa elimu na mwongozo wa jumla kuhusu muda unaohitajika kwa homoni ya ujauzito (hCG) kupungua baada ya kutoa mimba—iwe kwa dawa, kusafishwa, au mimba imetoka yenyewe. Kikokotoo hiki hakitoi jibu la moja kwa moja kama una mimba au huna mimba, bali kinaeleza kama muda uliopita unaweza kuathiri matokeo ya kipimo chako.


Kikokotoo hiki kinatumika kufanya mambo yafuatayo:

  • Kukadiria muda uliopita tangu utoe mimba

  • Kueleza kama hCG bado inaweza kuonekana kwenye kipimo cha mimba hivyo kusema mimba inawezekana kuwepo au la

  • Kukupa elimu ya muda wa kawaida wa kushuka kwa hCG (wiki 1–8) ambako kunaendana na majibu ya kipimo kusoma mimba ipo au la

  • Kukuonya kama umeshiriki ngono bila kinga baada ya kutoa mimba (kwani mimba mpya inaweza kutokea)

  • Kukupa ushauri wa jumla wa lini ni busara kupima tena

  • Kutoa elimu kuhusu matumizi ya kinga kama hupangi kupata mimba


Namna ya Kutumia Kikokotoo

  1. Weka tarehe uliyotoa mimba

  2. Weka tarehe uliyofanya kipimo cha ujauzito

  3. Weka idadi ya siku za mzunguko wako wa hedhi

  4. Chagua kama uliwahi kushiriki ngono bila kinga baada ya kutoa mimba

  5. Bonyeza “Kokotoa”

  6. Utaona maelezo juu ya kama muda uliopita unaweza kuathiri matokeo ya kipimo chako kutokana na mabaki ya homoni ya hCG.

  7. Utapata pia ushauri wa jumla kuhusu muda mzuri wa kupima tena na matumizi ya kinga.



ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

4 Februari 2026, 04:08:42

Rejea za mada hii

  1. Schreiber CA, Cahill EP, Castaño PM, et al. Low serum human chorionic gonadotropin levels after medication abortion: a systematic review. Contraception. 2019;99(2):77–83.

  2. Raymond EG, Grimes DA. The comparative safety of legal induced abortion and childbirth in the United States. Obstet Gynecol. 2012;119(2 Pt 1):215–9.

  3. Chen MJ, Creinin MD. Mifepristone With Misoprostol for Medical Abortion: A Systematic Review. Obstet Gynecol. 2015;126(1):12–21.

  4. Barnhart KT, Sammel MD, Rinaudo PF, Zhou L, Hummel AC, Guo W. Symptomatic patients with an early viable intrauterine pregnancy: do serum human chorionic gonadotropin values predict pregnancy outcome? Am J Obstet Gynecol. 2004;191(3):1059–64.

  5. Speroff L, Fritz MA. Clinical Gynecologic Endocrinology and Infertility. 8th ed. Philadelphia: Lippincott Williams & Wilkins; 2011.

  6. World Health Organization. Clinical practice handbook for quality abortion care. Geneva: WHO; 2022.

  7. National Institute for Health and Care Excellence (NICE). Abortion care guideline NG140. London: NICE; 2019.

  8. Mansour D, Gemzell-Danielsson K, Inki P, Jensen JT. Fertility after discontinuation of contraception: a comprehensive review of the literature. Contraception. 2011;84(5):465–77.

bottom of page