Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Imeboreshwa:
18 Julai 2025, 21:26:45

Kikokotoo cha Shinikizo la damu: Ushauri wa chakula na Mazoezi
Kikokotoo cha Shinikizo la Damu ni kifaa cha mtandaoni kinachosaidia watumiaji kutathmini hali ya shinikizo la damu kwa kuingiza vipimo vya systolic (juu) na diastolic (chini). Kikokotoo hutumia viwango vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na miongozo ya kimataifa kutambua hali ya mtumiaji kama ifuatavyo:
Shinikizo la kawaida: Systolic <120 mmHg na Diastolic <80 mmHg
Hatua ya kwanza ya ongezeko: Systolic 120–129 mmHg na Diastolic <80 mmHg
Shinikizo la damu hatua ya 1: Systolic 130–139 mmHg au Diastolic 80–89 mmHg
Shinikizo la damu hatua ya 2: Systolic ≥140 mmHg au Diastolic ≥90 mmHg
Hatari kubwa (Crisis): Systolic >180 mmHg au Diastolic >120 mmHg (inahitaji huduma ya dharura)
Faida za kikokotoo kiki
Kutathmini Hatari ya Afya – Husaidia watu kujua kama wako kwenye hatari ya shinikizo la damu.
Miongozo ya Lishe – Hutoa mpango wa chakula wa siku 7 kwa watu wenye ongezeko la BP ili kusaidia kudhibiti tatizo.
Miongozo ya Mazoezi – Hupendekeza mazoezi salama na rahisi ya kila siku (kama kutembea, yoga nyepesi).
Elimu ya Afya – Huongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kupima BP mara kwa mara.
Umuhimu
Shinikizo la damu ni kisababishi kikuu cha magonjwa ya moyo, kiharusi na figo. Watu wengi hawajui hali yao hadi tatizo lipate madhara makubwa. Kikokotoo hiki ni njia rahisi ya kujua hatari mapema na kuchukua hatua.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
18 Julai 2025, 20:37:54
Rejea za mada hii
Whelton PK, Carey RM, Aronow WS, Casey DE, Collins KJ, Dennison Himmelfarb C, et al. 2017 ACC/AHA/AAPA/ABC/ACPM/AGS/APhA/ASH/ASPC/NMA/PCNA Guideline for the Prevention, Detection, Evaluation, and Management of High Blood Pressure in Adults. Hypertension. 2018;71(6):e13–e115.
World Health Organization. Hypertension. Geneva: WHO; 2023. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/hypertension
Unger T, Borghi C, Charchar F, Khan NA, Poulter NR, Prabhakaran D, et al. 2020 International Society of Hypertension Global Hypertension Practice Guidelines. Hypertension. 2020;75(6):1334–1357.
James PA, Oparil S, Carter BL, Cushman WC, Dennison-Himmelfarb C, Handler J, et al. 2014 Evidence-Based Guideline for the Management of High Blood Pressure in Adults: Report from the Panel Members Appointed to the Eighth Joint National Committee (JNC 8). JAMA. 2014;311(5):507–520.
World Health Organization. STEPwise approach to surveillance (STEPS). Geneva: WHO; 2022. Available from: https://www.who.int/teams/noncommunicable-diseases/surveillance/systems-tools/steps
