Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
Imeboreshwa:
15 Mei 2025, 17:10:52

Kwa nini nimechelewa hedhi na ninapata vitone tu vya damu?
Swali
Hedhi yangu ilipaswa kuanza tarehe 12, lakini tarehe 13 nikaanza kuona vitone vidogo vya damu ambavyo si vya kuvaa pedi. Mpaka sasa hali hiyo haijabadilika – sipati hedhi ya kawaida. Shida inaweza kuwa nini?
Â
Jibu:
Kutokwa na damu kidogo (inayojulikana kama spotting) badala ya hedhi ya kawaida  huonekana kama matone madogo ya damu ya kahawia au nyekundu isiyohitaji pedi nzito. Hali hii mara nyingi hutokea siku chache kabla au baada ya hedhi, lakini pia inaweza kuashiria mabadiliko katika mzunguko wa hedhi
Visababishi vya kutokwa na vitone tu
Mabadiliko ya homoni
Matatizo katika viwango vya homoni za estrogeni na projesteroni yanaweza kusababisha mzunguko usio wa kawaida wa hedhi au kutokwa na damu kidogo tu.
Ujauzito
Kutoka vitone vya damu inaweza kuwa ishara ya ujauzito, hii ni kwasababu ya kujishikiza kwa kijusi katika mji wa mimba baada ya yai kurutubishwa.
Matumizi ya uzazi wa mpango
Vidonge vya kupanga uzazi, sindano, au vipandikizi vinaweza kusababisha damu isiyo ya kawaida, hasa katika miezi ya mwanzo ya matumizi.
Magojwa ya mfumo wa uzazi
Hali kama sindromu ya ovari yenye vifukomaj vingi, uvimbe faibroidi kwenye mji wa mimba, au utando wa ndani wa mfuko wa uzazi kuenea nje, huweza kuathiri mzunguko wa hedhi.
Maambukizi katika mfumo wa uzazi
Maambukizi ya mfumo wa uzazi huweza kusababisha kutokwa na damu isiyo ya kawaida.
Â
Unapaswa kufanya nini?
Fanya kipimo cha ujauzito, hasa kama ulishiriki ngono bila hukutumia njia ya uzazi wa mpango wakati wa uovuleshaji
Fuatilia mzunguko wako kwa karibu, unaweza kutumia kalenda au programu za simu
Onana na daktari wa afya ya uzazi endapo hali itaendelea kwa zaidi ya wiki au inajirudia mara kwa mara.
Â
Hitimisho
Kutokwa na vitone badala ya hedhi ya kawaida si jambo la kupuuzwa. Ingawa inaweza kuwa ya kawaida, pia inaweza kuwa dalili ya hali inayohitaji uchunguzi wa kitabibu. Ni muhimu kuchukua hatua mapema ili kuelewa chanzo chake na kupata matibabu sahihi.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
15 Mei 2025, 17:01:51
Rejea za mada hii
Munro, M.G., Critchley, H.O.D. & Fraser, I.S., 2018. Abnormal Uterine Bleeding. [online] NCBI Bookshelf. Available at: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK532913/. Imechukuliwa 15.05.2025
MSD Manuals, 2023. Abnormal Uterine Bleeding - Gynecology and Obstetrics. [online] Available at: https://www.msdmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/menstrual-abnormalities/abnormal-uterine-bleeding . Imechukuliwa 15.05.2025
Medscape, 2023. Abnormal (Dysfunctional) Uterine Bleeding. [online] Available at: https://emedicine.medscape.com/article/257007-overview. Imechukuliwa 15.05.2025
American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG), 2020. Abnormal Uterine Bleeding. [online] Available at: https://www.acog.org/womens-health/faqs/abnormal-uterine-bleeding. Imechukuliwa 15.05.2025
Mayo Clinic, 2023. Vaginal spotting: Causes. [online] Available at: https://www.mayoclinic.org/symptoms/vaginal-bleeding-between-periods/basics/causes/sym-20050756. Imechukuliwa 15.05.2025
NHS, 2023. Vaginal discharge and bleeding between periods. [online] Available at: https://www.nhs.uk/conditions/vaginal-discharge/. Imechukuliwa 15.05.2025
