Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
30 Mei 2025, 13:30:44

Kutema mate sana na kichefuchefu kwa mwanamke
Swali la msingi
Mke wangu anatema mate sana kwa wingi na anahisi kichefuchefu, je ni mimba?
Majibu
Wanawake wengi hupatwa na hali ya kutema mate kwa wingi na kichefuchefu, hasa wakiwa katika umri wa kuweza kupata mimba. Ingawa hizi ni dalili za kawaida katika miezi ya mwanzo ya ujauzito, kuna visababishi vingine vingi vya kitabibu ambavyo havihusiani na mimba. Makala hii inafafanua visababishi hivyo, dalili zinazoweza kuambatana navyo, pamoja na hatua za kuchukua.
Mimba kama kisababishi
Katika ujauzito, hasa wiki ya 6 hadi ya 12, ongezeko la homoni kama hCG na estrojeni husababisha mabadiliko yanayoathiri ladha, harufu, usagaji wa chakula, na mfumo wa neva — hali inayoweza kuchangia mate mengi na kichefuchefu.
Hali ya kutema mate kitaalamu huitwa ptyalism gravidarum.
Inaweza kuwa ya kudumu au ya muda mfupi.
Huambatana na homa ya asubuhi, upungufu wa hamu ya kula, na kichefuchefu.
Jedwali: Visababishi vya kutema mate kwa wingi na kichefuchefu
Kisababishi | Dalili zingine zinazoambatana | Ushauri wa Kitaalamu |
Mimba (Kipindi cha kwanza cha ujauzito) | Kukosa hedhi, uchovu, kuongezeka kwa harufu, mkojo mara kwa mara | Fanya kipimo cha mimba (hCG kwenye mkojo), onana na daktari wa kliniki ya wajawazito |
Vidonda vya tumbo (PUD) | Maumivu ya epigastrium, kiungulia, kutapika damu | Kipimo cha Helicobacter pylori, endoskopi, dawa za PPI |
Maambukizi ya tumbo na matumbo | Kuhara, homa, maumivu ya tumbo | Kunywa maji a kutosha, kupima kinyei maambukizi, kutumia dawakulingana na kisababishi |
Kipanda uso | Maumivu ya kichwa upande mmoja, mwanga kukera, kutapika | Dawa salama za maumivu, epuka vichocheo vya kipanda uso |
Sumu (organophosphates) | Kutokwa jasho, kuharisha, misuli kulegea, pupils kupungua | Tiba ya haraka hospitalini – atropine, pralidoxime |
Dawa (clozapine, opioids, chemo) | Kuhisi uzito, kutapika, usingizi mwingi | Dhibiti au badilisha dawa chini ya uangalizi wa daktari |
Maambukizi ya fizi au meno | Harufu mbaya mdomoni, maumivu ya fizi, kutokwa damu | Tiba ya meno, usafi wa kinywa |
Kisukari (DKA) | Kiu kupita kiasi, kukojoa mara kwa mara, pumzi ya harufu ya matunda, kuchanganyikiwa | Blood sugar test, tiba ya dharura hospitalini |
Homoni nyingi ya thairoidi kwenye damu | Mapigo ya moyo kasi, kupungua uzito, joto, kutetemeka | TSH na FT4 test, dawa za thyroid |
Msongo wa mawazo / wasiwasi | Kupumua kwa haraka, moyo kwenda mbio, kukosa usingizi | Ushauri wa kisaikolojia, relaxation techniques, counselling |
Kizunguzungu (vetigo) | Kuhisi kuzunguka, kupoteza usawa, kutapika | Tathmini ya ENT, tiba mazoezi ya neva vestibula |
Vipimo muhimu kufanya
Vipimo vya kugundua kisababishi ni pamoja na;
Kipimo cha haraka cha mimba kwa mkojo au damu – kudhibitisha au kukataa mimba.
Kipim cha damu cha sukari- Kuangalia kisukari.
Kipmo cha homni za tezi thairoidi TSH & FT4 – kuangalia homoni za thairoid.
Uchunguzi wa meno na fizi – kama kuna maambukizi ya mdomoni.
Picha kamili ya damu – kuangalia upungufu wa damu au maambukizi.
Ultrasound ya tumbo – kama kuna wasiwasi wa viungo vya ndani.
Nini cha kufanya?
Usikurupuke kuhitimisha kuwa ni mimba – hakikisha kwa kipimo.
Zingatia muda na mazingira ya dalili – zipo baada ya kula? Asubuhi pekee?
Tafuta msaada wa daktari – hasa kama dalili zinazidi au huchanganyika na kizunguzungu, homa, au kupungua uzito.
Epuka kujitibu bila ushauri wa kitaalamu – hasa kwa dawa za kichefuchefu au antibayotiki.
Endelea kufuatilia dalili – iandike kila siku ili kusaidia uchunguzi wa daktari.
Hitimisho
Kutema mate kwa wingi na kichefuchefu si lazima kumaanishe mimba. Ni dalili za kawaida zinazoweza kusababishwa na magonjwa mengi, dawa, au hali za kisaikolojia. Uchunguzi wa kina na vipimo sahihi vinahitajika ili kutoa majibu ya uhakika. Ikiwa unakabiliwa na hali hii au mpenzi wako anapitia dalili hizo, tafuta msaada wa kitabibu mapema ili kutambua chanzo na kuanza matibabu sahihi.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
30 Mei 2025, 13:33:21
Rejea za mada hii
Cunningham FG, Leveno KJ, Bloom SL, Spong CY, Dashe JS, Hoffman BL, et al. Williams Obstetrics. 25th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2018.
Erick M. Hyperemesis gravidarum: a review of recent literature. Pharm Pract (Granada). 2014 Oct-Dec;12(4):427.
Longo DL, Fauci AS, Kasper DL, Hauser SL, Jameson JL, Loscalzo J. Harrison’s Principles of Internal Medicine. 20th ed. New York: McGraw-Hill; 2018.
World Health Organization. Clinical guidelines on early pregnancy symptoms. Geneva: WHO; 2020.
ULY Clinic. Ptyalism gravidarum [Internet]. Dar es Salaam: ULY Health Services; [cited 2025 May 28]. Available from: https://www.ulyclinic.com