top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Glory M, MD

21 Machi 2025, 05:42:50

Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi

Nini husababisha kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi?

Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi ni hali ambapo mwanamke hupata damu kutoka ukeni nje ya kipindi chake cha kawaida cha hedhi. Hali hii inaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, maambukizi, au magonjwa makubwa kama saratani ya kizazi.


Makala hii imezungumzia kuhusu visababishi, dalili, uchunguzi, na Matibabu ya tatizo la tatizo la kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa Hedhi.

 

Kumbuka: Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi katika makala hii imemaanisha kutokwa na damu kipindi chochote kile kabla ya tarehe ya hedhi inayofuata kuwadia.


Visababishi vya kutokwa na damu katikati ya Hedhi

Kisababishi

Dalili

Uchunguzi

Matibabu

Mabadiliko ya Homoni

Mizunguko ya hedhi isiyo ya kawaida, matone ya damu kidogo kati ya hedhi

Vipimo vya homoni (FSH, LH, estrogen, progesterone), ultrasound

Vidonge vya kupanga uzazi, tiba ya homoni

Kutokwa na Damu Wakati wa Ovulation

Matone ya damu katikati ya mzunguko wa hedhi, maumivu ya wastani ya upande yai lilipotolewa

Historia ya hedhi, kufuatilia ovulation

Haihitaji matibabu maalumu

Ugonjwa wa Ovari yenye vifuko maji vingi (PCOS)

Hedhi isiyo ya kawaida, chunusi, unene, kuwa nanywele nyingi mwilini

Ultrasound ya nyonga, vipimo vya homoni

Mabadiliko ya mtindo wa maisha, dawa za homoni (OCPs, metformin)

Uvimbe kwenye Kizazi (Fibroid)

Hedhi nzito, maumivu ya nyonga, kukojoa mara kwa mara

Uchunguzi wa nyonga, ultrasound, MRI

Dawa za kupunguza uvimbe, upasuaji (Kuondoa uvimbe au kizazi)

Vinundu ndani ya mji wa mimba (Polyps)

Kutokwa na damu kati ya hedhi, hedhi nzito

Ultrasound, hysteroscopy

Upasuaji wa kuondoa vinundu

Endometriosis

Maumivu makali ya hedhi, maumivu ya nyonga, utasa

Laparoscopy, ultrasound

Dawa za kupunguza maumivu, tiba ya homoni, upasuaji

Maambukizi kwenye via vya uzazi (PID)

Maumivu ya nyonga, uchafu usio wa kawaida, homa, maumivu wakati wa ngono

Uchunguzi wa nyonga, vipimo vya maambukizi kwenye ute ukeni na Ultrosound

Antibiotiki, dawa za kupunguza maumivu

Saratani ya shingo ya kizazi au saratani ya kizazi

Kutokwa na damu baada ya hedhi, hedhi nzito, maumivu ya nyonga

Pap smear, biopsy, MRI

Upasuaji, tiba ya mionzi, kemotherapi

Magonjwa ya Zinaa (Klamidia, Kaswende, Kisonono, n.k.)

Uchafu ukeni wenye harufu mbaya, maumivu ya nyonga, damu baada ya tendo la ndoa

Vipimo vya magonjwa ya zinaa (PCR, culture)

Antibiotiki

Matumizi ya dawa za kuzuia mimba (IUD, Vidonge, sindano za depo-provera)

Kutokwa na damu isiyo ya kawaida, mzunguko wa hedhi kubadilika

Historia ya uzazi wa mpango, ultrasound kurekebisha mkao wa IUD

Kubadilisha njia ya uzazi wa mpango

Msongo wa mawazo na mtindo wa maisha

Hedhi isiyo ya kawaida, mabadiliko ya mhemko

Tathmini ya maisha na historia ya mgonjwa

Kudhibiti msongo wa mawazo, kula vizuri, kufanya mazoezi

Matumizi ya dawa (za kuyeyusha damu, Tiba ya Homoni, korticosteroids)

Kutokwa na damu isiyoeleweka

Historia ya matumizi ya dawa, vipimo vya damu

Kubadilisha au kurekebisha dawa


Uchunguzi wa Kutokwa na Damu Kati ya Hedhi

Ili kubaini chanzo cha tatizo, daktari anaweza kufanya mambo na vipimo vifuatavyo:


i) Historia ya Matibabu na uchunguzi wa kimwili
  • Historia ya mzunguko wa hedhi

  • Historia ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango

  • Dalili zinazofuatana na kutokwa damu (uchungu, homa, maumivu ya nyonga)


ii) Vipimo vya maabara
  • Kipimo cha damu (CBC) – Kutathmini upungufu wa damu (anemia) au maambukizi

  • Kupima mimba (hCG) – Kuthibitisha au kubaini ujauzito

  • Vipimo vya homoni – FSH, LH, estrogeni, progesterone, androjeni

  • Vipimo vya magonjwa ya inzaa – Kuangalia uwepo wa maambukizi ya Klamidia, kaswende na kisonono


iii) Uchunguzi wa picha na uchunguzi maalum
  • Ultrasound ya nyonga – Kubaini uvimbe, cysts, au matatizo ya uterasi

  • Hysteroscopy – Kuchunguza moja kwa moja ndani ya mji wa mimba

  • Biopsy ya Endometrium – Kuchukua sampuli ya ukuta wa kizazi kutathmini saratani

  • Pap Smear na Kipimo cha HPV – Kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi


Matibabu ya kutokwa na damu katikati ya hedhi

Matibabu ya kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo, baadhi yake huhusisha:

  • Tiba ya Homoni – Vidonge vya uzazi wa mpango, tiba ya homoni (GnRH analogs) kwa matatizo ya homoni, PCOS, na endometriosis.

  • Antibiotiki – Kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa au PID.

  • Upasuaji – Kuondoa fibroid, vinundu, tishu za endometria (endometriosis), au uvimbe wa saratani (kuondoa kizazi au sehemu ya kizazi).

  • Mabadiliko ya mtindo wa maisha – Kula chakula bora, kudhibiti uzito, kupunguza msongo wa mawazo.

  • Kurekebisha matumizi ya dawa – Ikiwa dawa fulani zinachangia au ksuabababisha tatizo, mfano dawa za kuyeyusha damu.


Wakati gani unapaswa kumwona Daktari unapotokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi?

Ni muhimu kutafuta msaada wa daktari ikiwa unapta hali na dalili zifuatazo;

  • Damu inatoka mara kwa mara katikati ya hedhi

  • Kutokwa na damu kunaambatana na maumivu makali ya nyonga, kizunguzungu, au homa

  • Unapata damu baada ya kufikia ukomo wa hedhi (komahedhi)

  • Kuna uchafu ukeni wenye harufu mbaya au maumivu baada ya tendo la ndoa

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

21 Machi 2025, 07:22:34

Rejea za mada hii

  1. Wise LA, Mikkelsen EM, Rothman KJ, Riis AH, Sorensen HT, Huybrechts KF, et al. A prospective cohort study of menstrual characteristics and time to pregnancy. American journal of epidemiology. 2011;174:701–9. doi: 10.1093/aje/kwr130.

  2. Harlow SD, Ephross SA. Epidemiology of menstruation and its relevance to women’s health. Epidemiologic reviews. 1995;17:265–86. doi: 10.1093/oxfordjournals.epirev.a036193.

  3. Direito A, Bailly S, Mariani A, Ecochard R. Relationships between the luteinizing hormone surge and other characteristics of the menstrual cycle in normally ovulating women. Fertility and sterility. 2013;99:279–85. doi: 10.1016/j.fertnstert.2012.08.047.

  4. Chiazze L, Jr, Brayer FT, Macisco JJ, Jr, Parker MP, Duffy BJ. The length and variability of the human menstrual cycle. Jama. 1968;203:377–80.

  5. Rowland AS, et al. Influence of medical conditions and lifestyle factors on the menstrual cycle. Epidemiology (Cambridge, Mass) 2002;13:668–74. doi: 10.1097/00001648-200211000-00011.

  6. Mikolajczyk RT, Louis GM, Cooney MA, Lynch CD, Sundaram R. Characteristics of prospectively measured vaginal bleeding among women trying to conceive. Paediatric and perinatal epidemiology. 2010;24:24–30. doi: 10.1111/j.1365-3016.2009.01074.x.

  7. Dasharathy SS, Mumford SL, Pollack AZ, Perkins NJ, Mattison DR, Wactawski-Wende J, et al. Menstrual bleeding patterns among regularly menstruating women. American journal of epidemiology. 2012;175:536–45. doi: 10.1093/aje/kwr356.

  8. Livingstone M, Fraser IS. Mechanisms of abnormal uterine bleeding. Human reproduction update. 2002;8:60–7. doi: 10.1093/humupd/8.1.60.

  9. Practice Committee of American Society for Reproductive Medicine. Myomas and reproductive function. Fertility and sterility. 2008;90:S125–30. doi: 10.1016/j.fertnstert.2008.09.012.

  10. Taylor E, Gomel V. The uterus and fertility. Fertility and sterility. 2008;89:1–16. doi: 10.1016/j.fertnstert.2007.09.069.

  11. Ferenczy A. Pathophysiology of endometrial bleeding. Maturitas. 2003;45:1–14. doi: 10.1016/s0378-5122(03)00068-9.

  12. Heitmann RJ, Langan KL, Huang RR, Chow GE, Burney RO. Premenstrual spotting of >/=2 days is strongly associated with histologically confirmed endometriosis in women with infertility. American journal of obstetrics and gynecology. 2014;211:358.e1–6. doi: 10.1016/j.ajog.2014.04.041.

bottom of page