Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
19 Aprili 2022 15:52:05

Kawaida mwanaume anatakiwa akojoe mara ngapi?
Kama ilivyo kwenye mambo mbalimbali ya kimaisha, kila mtu ana kawaida yake kwenye idadi ya kukojoa kwa siku.
Kwa watu walio wengi ikiwa pamoja na wanaume, ni kawaida kukojoa mara 6 hadi 7 katika muda wa masaa 24. Hata hivyo kukojoa mara 4 hadi 10 katika masaa 24 huweza kuwa kawaida kwa mtu mwenye afya njema na asiye na wasiwasi kuhusu idadi ya mara ngapi anaenda kukojoa.
Mambo yanayoathiri mara ngapi mwanaume anakojoa kwa siku( katika masaa 24)
Idadi ya mara ngapi unaenda kukojoa pia hutegemea mambo mbalimbali kama;
Kiasi cha maji unachaokunywa kwa siku mfano kunyw amaji mengi zaidi husababisha kukojoa mara kwa mara
Aina ya dawa unazotumia ( mfano dawa za kushusha shinikizo la damu kwa kupunguza maji mwilini hufanya ukojoe zaidi)
Aina ya vyakula unavyokula mfano vyakula vyenye kafeini kwa wingi husababisha kukojoa mara kwa mara
Magonjwa mfano kisukari, UTI na kuvimba kwa tezi dume huweza ongeza idadi ya mara ngapi unakojoa
Sababu zingine ambazo zimeorosheshwa kwenye video inayofuata
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
19 Aprili 2022 15:52:05
Rejea za mada hii
b&b comunity. Urinary Frequency – How Often Should You Pee?.https://www.bladderandbowel.org/bladder/bladder-conditions-and-symptoms/frequency/#:~:text=For%20most%20people%2C%20the%20normal,times%20they%20visit%20the%20toilet.Imechukuliwa 19.04.2021
MSD MANUAL Consumer Version. Urinary frequency. https://www.msdmanuals.com/home/kidney-and-urinary-tract-disorders/symptoms-of-kidney-and-urinary-tract-disorders/urination,-excessive-or-frequent?redirectid=11. Imechukuliwa 19.04.2021
Rakel RE, et al., eds. Urinary tract disorders.http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 19.04.2021
LeBlond RF, et al., eds. The urinary system.http://www.accessmedicine.com. Imechukuliwa 19.04.2021
Web MD. Frequent micturition. https://www.webmd.com/urinary-incontinence-oab/frequent-urination-causes-and-treatments#. Imechukuliwa 19.04.2021
Health partner. https://www.healthpartners.com/blog/frequent-urination-in-women-12-causes-and-how-to-get-help/. Imechukuliwa 19.04.2021