Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
10 Oktoba 2021, 12:30:45
Kwanini zimeletwa chanjo za J&J Tanzania na uko ziliwahi kuwa zinalalamikiwa na mataifa mengine?
Chanjo zote ni salama na zina ubora unaofaa kwa matumizi ya kila mtu bila kujali rangi na jinsia. Kuna uhaba mkubwa sana duniani wa chanjo ambapo kasi ya utengenezwaji hailingani na mahitaji halisi. Chanjo ya Janssen ina faida nyingi ikiwemo kuhitajika kwa dozi moja pekee hivyo kutokuhitaji mtu kuchomwa sindano mara mbili. Pia, chanjo hii inahitaji kutunzwa kwenye ubaridi wa kawaida wa kwenye jokofu na hivyo kuwezesha usambazaji hadi maeneo ya vijijini
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
10 Oktoba 2021, 12:30:45
Rejea za mada hii