top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021 11:09:14

Kwanini kuna chanjo nyingi za COVID-19?

Kwanini kuna chanjo za aina mbalimbali? Je zote zinamchanganyiko sawa?

Wakati mlipuko wa COVID-19 ulipotokea na watu kuathirika na kufa kwa wingi duniani kote, makampuni mbalimbali toka nchi mbalimbali yalianza juhudi za kufanya tafiti za kuvumbua chanjo za COVID-19. Hivyo baadhi ya makampuni yaliweza kuja na aina tofauti za chanjo ambazo baadae zilifanyiwa majaribio ya usalama na ufanisi wake. Na hii ndio chimbuko na uwepo wa aina tofauti tofauti za chanjo za COVID-19. Hata hivyo, uwepo huu wa chanjo za aina tofauti tofauti ni jambo jema kwani uhitaji wa chanjo wa COVID-19 duniani ni mkubwa sana, kiasi kwamba ingekuwa ni kuna aina moja tu ya chanjo inayotengenezwa na kampuni moja tu isingeweza kutengeneza chanjo za kutosheleza mahitaji duniani kote kwa wakati.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 12:27:59

Rejea za mada hii

bottom of page