Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
15 Julai 2023 13:46:25
Je magnesium salicylate inaweza kutumika na pombe?
Usinye dawa ya magnesium salicylate wakati unatumia pombe. Pombe huongeza hatari ya kuvia damu tumboni kunatotokana na dawa hii. Kama imetokea umefanya hivyo na unavuja damu tumboni, wasiliana na daktari wako mara moja.
Dalili zakuvia damu tumboni
Dalili za kuvia damu tumboni zinajumuisha:
Kutapika damu
Kupata choo cheusi
Kupata choo chenye damu
Kutapika matapishi rangi ya unga wa kahawa
Ni vema kuongea na daktari afahamu dawa zingine unazotumia ikiwa pamoja na vitamin na dawa za asili. Unashauriwa pia kutoacha dawa yoyote pasipo kuwasiliana na daktari wako kwanza.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
15 Julai 2023 13:49:00
Rejea za mada hii
Magnesium and alcohol interaction. https://www.drugs.com/food-interactions/magnesium-salicylate.html#:. Imechukuliwa 15.06.2023
Poikolainen K, Alho H. Magnesium treatment in alcoholics: a randomized clinical trial. Subst Abuse Treat Prev Policy. 2008 Jan 25;3:1. doi: 10.1186/1747-597X-3-1. Erratum in: Subst Abuse Treat Prev Policy. 2008;3:5. Dosage error in article text. PMID: 18218147; PMCID: PMC2265283.