top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Imeboreshwa:

13 Desemba 2025, 02:23:36

Magonjwa ya mwanaume yanayozuia kutungisha Mimba

Magonjwa ya mwanaume yanayozuia kutungisha Mimba

Kutotungisha mimba (ugumba wa mwanaume) ni hali ambapo mwanaume hushindwa kumtungisha mimba mwanamke baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga kwa kipindi cha angalau miezi 12. Takribani asilimia 40–50 ya visa vya wanandoa wanaoshindwa kupata ujauzito huhusisha tatizo kutoka kwa mwanaume, peke yake au kwa kushirikiana na mwanamke. Makala hii inaeleza magonjwa na hali za kiafya kwa wanaume zinazoweza kuathiri uwezo wa kutungisha mimba.


Kutotungisha mimba ni nini?

Kutotungisha mimba kwa mwanaume humaanisha kuwepo kwa tatizo kwenye:

  • Utengenezaji wa mbegu za kiume

  • Ubora au idadi ya mbegu

  • Usafirishaji wa mbegu

  • Uwezo wa kusimamisha au kumwaga shahawa

  • Uwiano wa homoni za uzazi


Jinsi uzazi wa mwanaume unavyofanya kazi

  • Mbegu hutengenezwa kwenye korodani

  • Homoni (hasa testosteroni) hudhibiti uzalishaji wa mbegu

  • Mbegu husafirishwa kupitia mirija (mrija wa vas deferensi)

  • Shahawa na manii hutolewa wakati wa kufika kileleni

Hitilafu katika hatua yoyote inaweza kuathiri uwezo wa kutungisha mimba.


Magonjwa yanayoathiri uwezo wa kutungisha mimba


1. Upungufu au ubora duni wa mbegu
  • Idadi ndogo ya mbegu

  • Mbegu zisizojogea vizuri

  • Mbegu zenye umbo lisilo la kawaida


Hii ni sababu kubwa zaidi ya utasa kwa wanaume.


2. Varikosili (Mishipa ya damu kwenye korodani kuvimba)
  • Husababisha joto kuongezeka kwenye korodani

  • Huathiri utengenezaji wa mbegu

  • Ni moja ya sababu zinazotibika kirahisi za kutotungisha mimba


3. Maambukizi ya njia ya uzazi(Magonjwa ya zinaa)
  • Kisonono

  • Klamidia

  • Epididymitis

  • ProstatitisMaambukizi haya yanaweza kuharibu mbegu au kuziba njia zake.


4. Kuziba kwa mirija ya mbegu (azoospermia ya kuziba)
  • Mbegu hutengenezwa lakini haziwezi kutoka nje ya mwili

  • Husababishwa na maambukizi, upasuaji au kasoro ya kuzaliwa kwenye njia za kupitisha mbegu nje ya mwili.


5. Matatizo ya homoni za uzazi
  • Upungufu wa testosteroni

  • Matatizo ya tezi ya pituitari au thairoid

  • Matumizi ya dawa au steroid


Homoni zisipo kuwa kwenye kiwango asilia, uzalishaji wa mbegu hupungua.


6. Matatizo ya kusimamisha au kumwaga shahawa
  • Matatizo ya kutosimamisha uume

  • Bao la ndani (Manii kurudi kwenye kibofu cha mkojo baada ya kutoka nje ya mwili). Hutokea hasa kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji unaohusisha tezi dume.

  • Kumwaga shahawa mapema sana au kutokuwepo kabisa


Hali hizi hupunguza idadi na nafasi ya mbegu zinazotakiwa kulifikia yai.


7. Magonjwa sugu ya mwili
  • Kisukari

  • Shinikizo la damu

  • Magonjwa ya figo au iniMagonjwa haya huathiri homoni, mishipa ya damu na nguvu za kiume.


8. Saratani na matibabu yake
  • Saratani ya korodani

  • Matibabu ya kemotherapia au radiotherapia


Haya yanaweza kuharibu kabisa uzalishaji wa mbegu.


9. Kasoro za kuzaliwa(Madhaifu ya kuzaliwa)
  • Sindromu ya Klinefelter

  • Kukosa korodani au kushuka kwa korodani kuchelewa


Hali hizi huathiri moja kwa moja uzazi wa mwanaume.


10. Mtindo wa maisha usiofaa

Ingawa si ugonjwa, huchangia sana:

  • Kuvuta sigara

  • Pombe kupita kiasi

  • Dawa za kulevya

  • Unene uliopitiliza

  • Joto kali la mara kwa mara kwenye korodani


Dalili za kutotungisha mimba kwa mwanaume

Mara nyingi hakuna dalili wazi, lakini zinaweza kujumuisha:

  • Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa

  • Maumivu au uvimbe wa korodani

  • Matatizo ya kusimamisha uume

  • Historia ya maambukizi ya uzazi (magonjwa ya zinaa)


Vipimo vya uchunguzi

  • Kipimo cha shahawa (Uchunguzi wa shahawa)

  • Vipimo vya homoni

  • Ultrasound ya korodani

  • Vipimo vya maambukizi

  • Vipimo vya vinasaba (kwa baadhi ya wagonjwa)


Matibabu ya kutotungisha mimba kwa mwanaume

Matibabu hutegemea chanzo kama yalivyoelezewa kwenye jedwali 1


Jedwali 1: Magonjwa ya mwanaume na matibabu yake

Tatizo/Mgonjwa

Athari kwa uzazi

Njia za matibabu

Idadi ndogo ya mbegu

Mbegu chache kufikia yai

Dawa za homoni, mabadiliko ya maisha

Ubora duni wa mbegu

Mbegu haziwezi kurutubisha yai

Viuajisumu, tiba ya msingi

Varikosili

Joto huua mbegu

Upasuaji wa varikosili

Maambukizi ya uzazi

Uharibifu wa mbegu/mirija

Antibayotiki

Kuziba kwa mirija

Mbegu haziwezi kutoka

Upasuaji au Njia saidizi za uzazi (Kutoa mbegu na kupandikiza kwenye kizazi cha mwanaumke au uchavushaji wa kwenye chupa)

Upungufu wa testosteroni

Uzazi hushuka

Tiba ya homoni

Erectile dysfunction

Mbegu hazifiki kwa yai

Dawa za nguvu za kiume

Kisukari

Huathiri mishipa na mbegu

Udhibiti wa kisukari

Saratani & tiba zake

Huua mbegu

Kuhifadhi mbegu kabla ya tiba kwa matumizi ya baadaye

Matatizo ya vinasaba

Mbegu hazitengenezwi

Uchavushaji yai kwenye chupa kwa kutumia mbegu za mtu mwingine au kuingiza mbegu za mtu mwingine kwenye kizazi cha mwanamke



Nini cha kufanya kama unashindwa kutungisha mimba?

  • Fika kliniki mapema

  • Chunguza wenza wote wawili

  • Epuka kujilaumu

  • Fuata ushauri wa daktari bingwa wa uzazi


Hitimisho

Kutotungisha mimba kwa mwanaume ni tatizo la kiafya linaloweza kutokea kwa mwanaume yeyote. Habari njema ni kwamba, sababu nyingi hutibika au kudhibitika endapo zitagundulika mapema. Uchunguzi wa kitaalamu na ushirikiano wa wanandoa ni msingi wa mafanikio.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

13 Desemba 2025, 02:23:36

Rejea za mada hii

  1. World Health Organization. Infertility [Internet]. Geneva: WHO; 2023 [cited 2025 Jan]. Available from:
    https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/infertility

  2. Centers for Disease Control and Prevention. Male infertility [Internet]. Atlanta (GA): CDC; 2023 [cited 2025 Jan]. Available from:
    https://www.cdc.gov/reproductivehealth/infertility/index.htm

  3. American Urological Association. Male infertility [Internet]. Linthicum (MD): AUA; 2022 [cited 2025 Jan]. Available from:
    https://www.auanet.org/guidelines/male-infertility

  4. Practice Committee of the American Society for Reproductive Medicine. Evaluation of the infertile male. Fertil Steril. 2020;113(1):37–45. Available from:
    https://www.fertstert.org/article/S0015-0282(19)32559-5/fulltext

  5. Mayo Clinic. Male infertility [Internet]. Rochester (MN): Mayo Foundation; 2023 [cited 2025 Jan]. Available from:
    https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/male-infertility/symptoms-causes/syc-20374773

  6. National Institute of Child Health and Human Development. What causes male infertility? [Internet]. Bethesda (MD): NICHD; 2022 [cited 2025 Jan]. Available from:
    https://www.nichd.nih.gov/health/topics/infertility/conditioninfo/causes/causes-men

bottom of page