top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Imeboreshwa:

20 Novemba 2025, 09:47:19

Magonjwa yanayoonekana kwa kupima damu

Magonjwa yanayoonekana kwa kupima damu

Kupima damu ni moja ya njia muhimu zaidi za kitabibu kutambua afya ya mwili na kugundua magonjwa mapema. Kipimo cha damu hutolewa kwa kuchukua kiasi kidogo cha damu kutoka sehemu mbalimbali za mwili kama mkononi, kichwani au miguuni


Baada ya damu kuchukuliwa, huchunguzwa maabara ili kubaini hali mbalimbali za mwili, utendaji wa viungo, maambukizi, na kiwango cha lishe.


Makala hii inaeleza magonjwa na hali muhimu zinazogundulika kupitia vipimo vya damu na maana yake kwa mgonjwa.


Ni magonjwa gani huonekana kwenye kipimo?

Kupima damu husaidia kubaini magonjwa mengi muhimu kama upungufu wa damu, kisukari, maambukizi, magonjwa ya figo, ini, tezi na matatizo ya moyo na mengine kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Ni kipimo rahisi lakini chenye taarifa pana kinachowezesha utambuzi wa mapema na kufuatilia maendeleo ya matibabu.


Jedwali: Magonjwa yanayogundulika kwa kupima damu

Kundi la ugonjwa

Vipimo vya damu vinavyofanyika

Maana ya matokeo / Tafsiri

1. Upungufu wa damu (Anemia)

Hemoglobin (Hb), RBC, Hematocrit

Viwango vya chini huonyesha upungufu wa damu kutokana na ukosefu wa madini, lishe duni, kutokwa damu au magonjwa ya figo.

2. Maambukizi ya bakteria/virusi

Chembe nyeupe za damu, chembe nyekundu za damu, CRP, ESR, Kuotesha vimelea

Chembe nyeupe ne CRP vikipanda huashiria mwili kupambana na maambukizi kama maambukizi ya njia ya mkojo, Nimonia, Sepsis.

3. Kisukari (Diabetes)

Kipimo cha sukari wakati wa mfungo, au sukari wakati usio wa mfungo, HbA1c

Viwango vya juu vinaonyesha kisukari au hatari ya kupata kisukari.

4. Magonjwa ya figo

Kreatinine, Yurea (BUN), Elektrolaiti

Kreatinine na yurea vikipanda huonyesha figo kushindwa kufanya kazi vizuri.

5. Magonjwa ya ini

ALT, AST, Bilirubin, ALP, Albumin

Viwango visivyo kawaida vinaonyesha hepataitis, Ini mafuta, ulevi, au Sirosisi.

6. Mafuta mwilini (Kolesterol-Lehemu)

Kiwango cha jumpa cha kolestrol, LDL, HDL, Triaiglaiseraid

LDL na traiglaiseride kuwa juu huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.

7. Magonjwa ya tezi (Tharoid)

TSH, T3, T4

TSH juu = Ugonjwa wa upunfugu wa homoni thairoidi; TSH chini = Wingi wa homoni thairoidi.

8. Malaria na minyoo

M=Kipimo cha maleria, Hesabu kamili ya damu na, Eosinophils

Malaria hupatikana moja kwa moja; eosinophils juu huashiria minyoo au mizio.

9. Kuganda kwa damu (Madhaifu ya ugandaji wa damu)

Chembe sahani za damu, INR, PT/APTT

Viwango visivyo kawaida vinaonyesha hatari ya kutokwa damu au kuganda kwa damu kupita kiasi.

10. Magonjwa ya moyo (mshituko wa moyo)

Troponin, CK-MB

Viwango vikiongezeka vinaonyesha uharibifu wa misuli ya moyo.

11. Saratani fulani (Viashiria saratani)

Kemikali viashiria saratani kwenye damu kama PSA, CEA, CA-125, AFP

Hutumika kufuatilia au kutilia shaka uwepo wa baadhi ya saratani.


Hitimisho

Ni muhimu kuelewa kuwa hakuna kipimo kimoja cha damu kinachoweza kugundua magonjwa yote. Kila kipimo kina jukumu lake na huwa na gharama tofauti kulingana na tatizo linalotafutwa. Kwa hiyo, kabla ya kuamua kupima, ni vyema kuzungumza na daktari ili akushauri vipimo sahihi vya kufanya kulingana na dalili zako na historia yako ya afya. Hii hukusaidia kuepuka gharama zisizo za lazima na kupata majibu sahihi zaidi.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

20 Novemba 2025, 09:47:19

Rejea za mada hii

  1. McPherson RA, Pincus MR. Henry’s Clinical Diagnosis and Management by Laboratory Methods. 24th ed. Philadelphia: Elsevier; 2022.

  2. Fischbach F, Dunning MB. A Manual of Laboratory and Diagnostic Tests. 10th ed. Philadelphia: Wolters Kluwer; 2021.

  3. American Association for Clinical Chemistry (AACC). Understanding laboratory tests [Internet]. 2024 [cited 2025 Nov 20]. Available from: https://labtestsonline.org

  4. Jameson JL, Fauci AS, Kasper DL, Hauser SL, Loscalzo J, editors. Harrison’s Principles of Internal Medicine. 21st ed. New York: McGraw Hill; 2022.

  5. Hoffbrand AV, Higgs DR, Keeling DM, Mehta AB. Postgraduate Haematology. 7th ed. Hoboken: Wiley Blackwell; 2016.

  6. World Health Organization. Laboratory services in primary healthcare. Geneva: WHO; 2021.

bottom of page