top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

20 Novemba 2021 18:25:35

Majira kwa anayetumia sigara

Je, Unaweza tumia majira wakati unavuta sigara?

Je, unavuta sigara na unataka kutumia majira yeney vichocheo viwili?

Kama unavuta sigara na unatamani kutumia vidonge vya majira, unapaswa kufahamu una umri gani.


Umri zaidi ya miaka 34

Kama una umri zaidi ya miaka 34 na unavuta sigara, usitumie vidonge vya majira vyenye vichocheo viwili. Unashauriwa kuacha kuvuta sigara au kuchagua njia nyingine.


Kwanini usitumie majira ya vidonge viwili pamoja na sigara?


Kutumia vidonge vya majira vyenye vichocheo viwili huongeza hatari zaidi ya kupata magonjwa ya mishipa ya damu, moyo na shinikizo la juu la damu kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 34.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021 18:25:35

Rejea za mada hii

bottom of page