top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Peter A, MD

20 Novemba 2021, 19:10:10

Majira kwa mwenye kiharusi

Je unaweza kutumia majira yenye vichocheo viwili kama una kiharusi?

Hapana!

Majira yenye vichocheo viwili haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye;


  • Kiharusi sasa

  • Historia ya kiharusi

  • Historia ya damu kuganda miguuni au kwenye mapafu

  • Historia ya moyo kushindwa kufanya kazi kutokana na damu kuganda kwenye mishipa ya moyo

  • Wenye matatizo mengine makubwa ya moyo


Njia gani unapaswa kutumia?


Kama una kiharusi au historia ya magonjwa ya mishipa ya damu kutokana na damu kuganda unapaswa kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango badala ya majira yeney vichocheo viwili. Unashauriwa kutotumia pia njia za uzazi wa mpango zenye kichocheo cha estrojeni au sindano ya projestini.


Kama una historia ya kuganda kwa damu ufanyaje?


Kama una historia ya kuganda kwa damu miguuni au kwenye mapafu, usitumie njia ya uzazi wa mpango yenye ichocheo chochote kile.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021, 19:10:10

Rejea za mada hii

  1. Bousser MG, et al. Oral contraceptives and stroke. Cephalalgia. 2000 Apr;20(3):183-9. doi: 10.1046/j.1468-2982.2000.00040.x. PMID: 10997772.

  2. AHA journals. Oral Contraceptives and Ischemic Stroke Risk. https://doi.org/10.1161/STROKEAHA.117.020084Stroke. 2018;49:e157–e159. Imechukuliwa 20.11.2021

  3. Li, Feng et al. “Oral Contraceptive Use and Increased Risk of Stroke: A Dose-Response Meta-Analysis of Observational Studies.” Frontiers in neurology vol. 10 993. 23 Sep. 2019, doi:10.3389/fneur.2019.00993

bottom of page