top of page

Mwandishi:

Dkt. Peter A, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

20 Novemba 2021, 19:35:50

Majira kwa mwenye kipanda uso

Je, unaweza tumia majira yenye vichocheo viwili kama una kipanda uso?

Hapana!

Kama una kipanda uso au unapata dalili za kipanda uso kama vile kushindwa kuona vema na maumivu makali ya kichwa ya kugonga upande mmoja wa kichwa na zingine hupaswi kutumia majira yenye vichocheo viwili.


Dalili za kipanda uso


Dalili zingine za kipanda uso ambazo zikufanye kutotumia vidonge vya majira yeney vichocheo viwili ni;


  • Kushindwa kuona kwa wakati

  • Maumivu makali ya kichwa

  • Maumivu ya kichwa ya kugonga kwa masaa kadhaa upande mmoja wa kichwa

  • Maumivu ya kichwa yanayoambatana na kichefuchefu au kutapika

  • Maumivu ya kichwa yanayozidi kwa ukiwa kwenye mwanga, kelele, au kutembea, au kujitikisa


Kwanini usitumie majira yenye vichocheo viwili kama una kipanda uso?


Majira yenye vichocheo viwili huamsha dalili za kipanda uso na kufanya upatwe na ugonjwa huu mara kwa mara. Hii ndio maana haishauriwi kutumika kwa wanawake wenye kipanda uso chenye aura au kisicho na aura au kama una umri wa miaka 35 au zaidi.


Kama una umri wa chini ya miaka 35 na una kipandauso bila aura, unaweza kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021, 19:35:50

Rejea za mada hii

  1. AHS. Migraine and Contraceptives. https://americanheadachesociety.org/news/migraine-contraceptives/#. Imechukuliwa 20.11.2021

  2. Allais G, et al. Oral contraceptives in migraine. Expert Rev Neurother. 2009 Mar;9(3):381-93. doi: 10.1586/14737175.9.3.381. PMID: 19271947.

bottom of page