Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Charles W, MD
19 Novemba 2021, 19:05:39

Je, kama una tatizo la shinikizo la juu la damu unaweza kutumia vidonge vya majira?
HAPANA
Kama una shinikizo la juu la damu, una historia ya shinikizo la juu la damu, au kama unapata matibabu ya shinikizo la juu la damu unashauriwa kutumia njia zingine za uzazi wa mango mbali na vidonge vyenye vichocheo viwili au sindano zenye estrojeni na progestin.
Pima shinikizo la damu kama inawezekana:
Kama shinikizo lako la damu litakuwa chini ya 140/90 mm Hg, unaweza tumia vidonge vyenye vichocheo viwili.
Kama shinikizo lako la damu la sistoli ni 140 mm Hg au zaidi au shinikizo la damu la diastoli likiwa 90 au zaidi, usitumie vidonge vyenye vichocheo viwili.
Ongea na mtaalamu wa afya akusaidie kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni, lakini isiwe sindano za projestini kama shinikizo la damu ni 160 au zaidi au shinikizo la diastoli ni 100 au zaidi.
Kumbuka
Ukipimwa mara moja shinikizo la damu na likakutwa lipo kati ya 140–159/90–99 mm Hg haitatosha kutambua shinikizo la juu la damu. Utapatiwa njia mbadala ya kutumia mpaka utakaporudi kwa ajili ya kupima tena shinikizo la damu, au utashauriwa kuchagua njia nyingine kama utakayopenda. Utakaporudi na kupimwa na kukutwa na shinikizo la damu chini ya 140/90, unaweza kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
19 Novemba 2021, 19:05:39
Rejea za mada hii
Oparil S. Hypertension and oral contraceptives. J Cardiovasc Med. 1981 Apr;6(4):381, 384-7. PMID: 12263383.
Afshari, et al. “Oral contraceptives and hypertension in women: results of the enrolment phase of Tabari Cohort Study.” BMC women's health vol. 21,1 224. 28 May. 2021, doi:10.1186/s12905-021-01376-4