top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

20 Novemba 2021 19:59:17

Majira na upasuaji mkubwa

Je, majira inaweza kutumika kwa mtu anayepanga kufanya upasuaji mkubwa?

Kama umepangiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utakufanya usitembee kwa wiki moja au zaidi, tumia njia zingine za uzazi wa mpango kama kinga badala ya vidonge vya majira vyenye vichocheo viwili.


Kwanini usitumie majira yenye vichocheo viwili kama unafanyiwa upasuaji mkubwa?


Upasuaji mkubwa unaokufanya usitembee unaongeza hatari ya damu kuganda. Kwa vile vidonge vya majira pia huongeza hatari ya damu kuganda, hatari hiyo huongezeka zaidi kiasi cha kukufanya upatwe na tatizo la damu kuganda. Usitumie dawa za majira kama unapanga kufanyiwa upasuaji mkubwa n ahata baada ya kumaliza wiki mbili baada ya kufanyiwa upasuaji, tumia kinga kwanza ndipo uendelee au kuanza vidonge vya majira.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021 19:59:17

Rejea za mada hii

  1. Anmol Chattha, et al. Oral Contraceptive Management in Aesthetic Surgery: A Survey of Current Practice Trends, Aesthetic Surgery Journal, Volume 38, Issue 3, March 2018, Pages NP56–NP60, https://doi.org/10.1093/asj/sjx234. Imechukuliwa 20.11.2021

  2. Hutchison GL. Oral contraception and post-operative thromboembolism: an epidemiological review. Scott Med J. 1989 Dec;34(6):547-9. doi: 10.1177/003693308903400601. PMID: 2698507.

  3. Sue-Ling H, et al. Should the pill be stopped preoperatively? Br Med J (Clin Res Ed). 1988 Feb 13;296(6620):447-8. doi: 10.1136/bmj.296.6620.447. PMID: 3126855; PMCID: PMC2545036.

bottom of page