Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
Imeboreshwa:
5 Juni 2025, 07:29:03

Maumivu ya korodani moja na ya wakati wa kukojoa: Je, ni gonorrhoea?
Swali la msingi
Habari doctor ninaumiri wa miaka 22 ni mwanaume toka wiki tatu zilizo pita nimeanza kuisi dalili za ugonjwa wa gonorrhoea ambayo ninaisi maumivu ya kolodani moja ya upande wa kulia pia maumivu ya kibofu cha mkojo wakati nikikojoa lakini pia wakati mwingine maumivu ya tumbo chini ya kitovu toka nimeanzaa kuisi ivyo sijatumiaa dawa yoyote ivyo naomb unisaidie dawa ili niweze tumia.
Majibu
Shukrani kwa kuwasiliana. Dalili unazozieleza—kama vile maumivu ya korodani upande mmoja, maumivu wakati wa kukojoa, na maumivu ya chini ya tumbo—zinaweza kuashiria maambukizi ya zinaa, hasa gonorrhoea au hata klamydia (ambayo mara nyingi huambatana pamoja). Maambukizi haya pia yanaweza kusababisha uvimbe kinga wa mrija wa korodani, hususan kwa wanaume vijana.
Kwa kuwa hujatumia dawa yoyote hadi sasa, na una dalili zinazodumu kwa zaidi ya wiki tatu, ni muhimu uanze matibabu mara moja, lakini pia upate uchunguzi wa kitaalamu ili kuthibitisha maambukizi na kuchunguza uwezekano wa maambukizi mengine ya magonjwa ya zinaa yanayofanana dalili na gono.
Matibabu ya awali ya gonorrhoea (kwa watu wazima)
Kulingana na miongozo ya WHO na CDC na mwongozo wa matibabu ya Tanzania wa Wizara ya afya wa mwaka 2021. Dawa hizi hutumika endapo gono imethibitishwa kuwa ndo chanzo cha tatizo. Wasiliana na daktari wako kwa dozi kamili.
Chaguo la kwanza la dawa (hutolewa pamoja)
Ceftriaxone mbadala wake ni Cefixime
Doxycycline mbadala wake ni Azithromycin
Kwa maumivu
Kama maumivu hayavumiliki dawa za kupunguza maumivu kama paracetamol au diclofenac hutumika kudhibiti maumivu wakati dawa za kutibu tatizo zinaendelea kutumika.
Mambo ya muhimu kuzingatia
Usifanye tendo la ndoa au ngono hadi utakapomaliza tiba na dalili kuisha.
Mshauri mpenzi wako au wapenzi wako wapimwe na watibiwe pia, hata kama hawana dalili.
Fanya vipimo vya magonjwa mengine ya zinaa, kama vile:
HIV
Syphilis
Hepatitis B na C
Lini umwone daktari haraka?
Ikiwa korodani inaendelea kuvimba au kuwa na maumivu makali.
Ikiwa una homa, kichefuchefu, au maumivu makali ya tumbo.
Ikiwa baada ya kutumia dawa dalili hazipungui baada ya siku 3–5.
Hitimisho
Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa afya aliyesajiliwa. Matumizi mabaya ya dawa yanaweza kusababisha kushindwa kupona, madhara ya kiafya, au kuibuka kwa vijidudu sugu. Tafadhali fika kwenye kituo cha afya kwa uchunguzi kamili na tiba sahihi kulingana na hali yako.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
18 Mei 2025, 15:51:58
Rejea za mada hii
World Health Organization. Sexually transmitted infections (STIs) [Internet]. Geneva: WHO; 2022 [cited 2025 May 18]. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/sexually-transmitted-infections-(stis)
Ministry of Health, Tanzania. National Guidelines for the Management of Sexually Transmitted and Reproductive Tract Infections. 4th ed. Dodoma: MoHCDGEC; 2021.
Workowski KA, Bachmann LH, Chan PA, Johnston CM, Muzny CA, Park I, et al. Sexually transmitted infections treatment guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187. doi:10.15585/mmwr.rr7004a1
Horner PJ, Blee K, O’Mahony C, Muir P. Diagnosis and management of epididymo-orchitis. BMJ. 2015;351:h3527. doi:10.1136/bmj.h3527
Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Gonorrhea - CDC Fact Sheet (Detailed) [Internet]. Atlanta: CDC; 2023 [cited 2025 May 18]. Available from: https://www.cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea-detailed.htm
Hook EW, Handsfield HH. Gonococcal infections in the adult. In: Holmes KK, Sparling PF, Stamm WE, editors. Sexually Transmitted Diseases. 4th ed. New York: McGraw-Hill; 2008. p. 627–645.
