top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

12 Oktoba 2021, 05:14:52

Muda wa chanjo ya COVID-19 kuanza kufanya kazi

Baada ya muda gani chanjo ya COVID-19 inaanza kufanya kazi baada ya kuchoma?

Muda wa kuanza kufnaya kazi hutofautiana kati ya chanjo na chanjo


Janssen

Tafiti za tafiti kwa binadamu zinaonyesha kuwa chanjo ya J&J/Janssen dhidi ya COVID-19 ilikuwa na uwezo wa kuzuia ugonjwa mkali na kulazwa kwa asilimia 66.3% kwa watu ambao hawakuwa na maambukizi ya awali ya COVID-19, ulinzi huu ulianza muda wa wiki mbili baada ya kuchoma chanjo. Hata hivyo tafiti za mwisho zimeonyesha uwezo wake mkubwa huonekana baada ya siku 28 tangu kuchoma chanjo.


Baadhi ya taarifa kwenye tafiti zinaonyesha kuwa chanjo hii inaweza kudumu kwenye damu kwa muda wa miezi tisa.


Pfizer

Taarifa za Chanjo ya Pfizer kutokana na tafiti za tafiti kwa binadamu zinaonyesha kuwa uwezo wa chanjo hii kupunguza ugonjwa mkali na kulazwa ni wa asilimia 91 katika miezi 4 ya mwanzo baada ya kupokea dozi ya pili ya chanjo licha ya uwezo huo kupungua mpaka asilimia 77 mara baada ya siku 120.


Moderna

Taarifa za tafiti kwa binadamu zinaonyesha kuwa Chanjo ya Moderna’s ufanisi wake wa kumlinda mtu kuugua ugonjwa mkali na kulazwa hospitali ni wa asilimia 93, uwezo huu hupungua mpaka asilimia 92 baada ya siku 120 kupita.



ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Oktoba 2021, 05:26:19

Rejea za mada hii

bottom of page