top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

3 Oktoba 2024, 11:49:34

Mzunguko wa hedhi ukoje?

Mzunguko wa hedhi ukoje?

Mzunguko wa hedhi ni mzunguko unao anza pale mwanamke anapoanza kuona damu ya hedhi katika mwezi. Kwa kawaida mara nyingi mzunguko huu huanza katika umri wa miaka 12. Baadhi ya wanawake wachache wanaweza kuona hedhi kabla au baada ya umri huo. Kipindi hiki cha hedhi ni pale ambacho mwanamke ameshapevuka yaani anakuwa tayari amepata nywele kwenye viungo vya siri, titi kukua, sauti kuwa nyororo n.k.

 

Kwa kawaida mzungukoo wa hedhi hutokea kati ya siku 21-35 na siku za kuona damu (bleeding) ni kuanzia siku 3-10 kwa wastani na kiwango cha damu kinachopotea kinakadiliwa kuwa ni mililita 30 hadi 40 na mzunguko wa hedhi kubadilika ni kawaida ndani ya miaka 2  ya kuanza hedhi kwa sababu tofauti tofauti.

 

Siku zipi mwanamke anakuwa hatarini kupata mimba?

Kutokana na maelezo ya mzunguko wa hehi hapo juu, siku za hatari yaani mwanamke anapoweza kupata mimba hutegemea idadi ya siku za mzunguko wa hedhi. Mfano mwanamke toka aone damu ya mwezi uliopita na hii ya sasa amechukua siku 28, tunaweza kusema mzunguko wake unachukua siku 28.

 

Siku ya 12 toka ulipoanza kuona damu hapo ndipo siku za hatari huanza na kumalizika siku tano zinazofuata yaani kutoka siku ya 12 hadi 17, hivo kipindi hiki cha hatari ni siku tano tu katika mzunguko mzima wa hedhi na haijalishi unaona damu kwa siku ngapi (yani kuanzia mara 3,4,5 n.k) kuhesabu siku za hatari unaweza kutumia njia hii.

 

Kumbuka: siku ya 14 ndio katikati ya mzunguko na hivo maranyingi yai la kike huwa limeshatolewa kiwadnani na kuwa katika mirija ya uzazi na hivo mbegu ya kiume kama ipo kwa wakati huo mimba hutungishwa.



Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mzunguko wa hedhi na siku ya hatari kupata mimba?

Pata maelezo zaidi katika makala ya tarehe ya kushika mimba na Kikokoteo cha umri wa ujauzito. sambamba na kuwasiliana na daktari wako kwa maelezo zaidi.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

3 Oktoba 2024, 11:56:34

Rejea za mada hii

  1. Kaunitz A. Abnormal uterine bleeding in nonpregnant reproductive-age women: Terminology, evaluation, and approach to diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 02.10.2024

  2. Welt C. Evaluation of the menstrual cycle and timing of ovulation. https://www.uptodate.com/contents/search. 02.10.2024

  3. Your menstrual cycle. Office of Women's Health. https://www.womenshealth.gov/menstrual-cycle/your-menstrual-cycle. 02.10.2024

  4. Period problems. Office of Women's Health. https://www.womenshealth.gov/menstrual-cycle/period-problems. 02.10.2024

  5. Melmed S, et al. Physiology and pathology of the female reproductive axis. In: Williams Textbook of Endocrinology. 14th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. 02.10.2024

  6. Welt CK. Normal menstrual cycle. https://www.uptodate.com/contents/search. 02.10.2024

bottom of page