Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Adolf, L, M.D
19 Julai 2023, 18:31:52
Ufanye nini ukifanya ngono zembe wakati unatumia PEP
Hili ni swali la msingi ambalo huulizwa na watumiaji wa PEP. Jambo la msingi kufahamu ni aina gani ya PEP unayotumia na umetumia kwa muda gani kabla ya kushiriki ngono.
Kama unatumia mchanganyiko wa PEP wenye dawa tenofovir DF/FTC (Truvada) na una muda wa siku 7 au zaidi, unaweza kulindwa dhidi ya maambukizi mengine ya VVU endapo utashiriki ngono zembe. Hata hivyo itategemea pia aina ya virusi na mwitikio wake kwenye dawa hii.
Licha ya kuwa na mjadala endelevu kuhusu mada hii, wataalamu wengi hukubali kuwa, matumizi ya PEP yenye tenofovir DF/FTC (Truvada) kwa siku 7 au zaidi hutengeneza ulinzi sawa na mtu anayetumia PrEP
Ufanye nini kama una hatari endelevu?
Kama una hatari endelevu ya kupata maambukizi, CDC inashauri kutumia PrEP badala ya PEP Â ili kupunguza hatari hiyo.
Magonjwa mengine unaypaswa kuogopa?
Mbali na kujikinga na maambukizi ya VVU, unapaswapia kufikiria uhusu magonjwa mengine ya zinaa kama gono, kaswende, klamidia, kirusi cha homa y aini na kirusi papilloma.
Unapaswa kutumia kinga kama hujui hali ya maambukizi ya yule unayeanya naye. Pia kupima na kupata chanjo ya kirusi cha homa y aini A na B na Papilloma anayeathiri binadamu hushauriwa kufnayika.
Kama umeshiriki ngono siku tofauti na zilizoelezwa hapa ufanyaje?
Kama itakuwa umeshiriki ngono siku tofauti na zilizoelezwa hapa au unatumia PEP yenye mchanganyiko tofauti na Truvada, wasiliana na daktari wako mara moja kwa ushauri na tiba. Daktari anaweza kukushauri kuendelea na dozi ya PEP kwa muda zaidi ya siku 28 kama umejiweka kwenye kihatarishi kingine.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Unaweza kupata maelezo kw akubofya makala zifuatazo;
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 19:43:17
Rejea za mada hii
CDC.Post-Exposure Prophylaxis (PEP) | HIV Risk and Prevention https://www.cdc.gov/hiv/risk/pep/index.html. Imechukuliwa 18.07.2023
NCBI. HIV Prophylaxis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK534852/#. Imechukuliwa 18.07.2023
NCBI. PEP to Prevent HIV Infection. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK562734/. Imechukuliwa 18.07.2023
PEP. http://publichealth.lacounty.gov/dhsp/Biomedical/Basics_of_PEP_for_Patient-EN_12.29.2021.pdf. Imechukuliwa 18.07.2023
PEP Information. https://www.alfredhealth.org.au/images/resources/patient-resources/PEP-Information.pdf. Imechukuliwa 18.07.2023