Mwandishi:
Dkt. Charles W, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
12 Oktoba 2021, 19:47:01

Ni dawa gani nzuri ya kushusha presha kwa ujauzito wa mwezi mmoja na nusu?
Presha au shinikizo la juu la damu ni moja ya tatizo maarufu kutokana na ujauzito lenye changamoto kwenye matibabu yake kutokana na madhara ugonjwa na dawa kwa kichanga.
Malengo ya kushusha shinikizo la damu kwenda 120/80 mmHg inaweza kuwa ya faida kwa mama, hata hivyo inapaswa kuchukuliwa umakini kwa kuwa dawa zinaweza kusababisha madhaifu ya kiuumbaji(ulemavu) kwa mtoto. Baadhi ya madhara yanaweza yasionekane mapema zaidi bali kuonekana miaka kadhaa baada ya mtoto kuzaliwa.
Baadhi ya dawa zenye taarifa nyingi kuhusu usalama wake wakati wa ujauzito na zinazotumika sana wakati wa ujauzito kushusha shinikizo la juu la damu ni;
Methyldopa
Licha ya dawa hizi kuwa na usalama mkubwa ukilinganisha na dawa zingine, dawa hizi zinapaswa kutumika kama faida ni kubwa kuliko madhara kwenye ujauzito.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
12 Oktoba 2021, 20:52:16
Rejea za mada hii
Wright JT Jr, et al. A randomized trial of intensive versus standard blood‐pressure control. N Engl J Med. 2015;373:2103–2116.
ACOG practice bulletin no. 203 summary: chronic hypertension in pregnancy. Obstet Gynecol. 2019;133:215–219.
Brown MA, et al. Hypertensive disorders of pregnancy: ISSHP classification, diagnosis, and management recommendations for international practice. Hypertension. 2018;72:24–43.
Magee LA, et al. Less‐tight versus tight control of hypertension in pregnancy. N Engl J Med. 2015;372:407–417.
Ankumah NA, et al. Risk of adverse pregnancy outcomes in women with mild chronic hypertension before 20 weeks of gestation. Obstet Gynecol. 2014;123:966–972.
Malha, et al. “Safety of Antihypertensive Medications in Pregnancy: Living With Uncertainty.” Journal of the American Heart Association vol. 8,15 (2019): e013495. doi:10.1161/JAHA.119.013495.