top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dr.Adolf S, MD.

1 Februari 2024 13:30:05

Ni zipi dalili za mtoto kushuka kwa ajili ya kutoka (kuzaliwa)?

Je, nitajuaje kama mtoto ameanza kushuka kwaajili ya kutoka?

Katika wiki za mwisho za ujauzito mtoto huanza kushuka kuingia katika nyonga ya uzazi tayari kwa kuzaliwa.

Hatua hii ni muhimu sana japo haimaanishi  kuwa leba itaanza mara moja. Mjamzito ni vema kufahamu dalili na viashiria vya mtoto kushuka katika nyonga.

Dalili za mtoto kushuka

Zifuatazo ni dalili na viashiria vya mtoto kushuka katika nyonga;

 • Kukojoa mara kwa mara

 • Kuhisi mgandamizo mkubwa kwenye nyonga

 • Kushindwa kutembea vema

 • Kuhisi maumivu ya via vya uzazi, kiuno  na mgongo

 • Kukosa haja kubwa au  kutoka kwa shinda

 • Kuongezeka kwa ute ukeni

 • Kupungua au kupotea kwa hali ya kupumua kwa shida

 • Kupungua au kupotea kwa dalili za kiungulia

 • Kupata bawasili

 • Tumbo la ujauzito kuonekana limeshuka

 

Nini cha kufanya

Unaweza kuendelea kufanya mazoezi ya kuanzisha uchungu ili kumsaidia mtoto kujiweka vema anaposhuka, na pia kuuandaa mwili wako kwa hatua ya leba.

Kumbuka

 • Kushuka kwa mtoto haimaanishi uchungu utaanza mara baada tu ya kushuka

 • Dalili tajwa hapo juu haziwezi kutokea endapo mtoto hajageuka na kutanguliza kichwa

 • Muda wa mtoto kushuka hutofautiana kati ya mjamzito mmoja na mwingine, kwani wajawazito wengine huanza kuona dalili siku kadhaa kabla ya leba kuanza na wengine masaa machache kabla ya leba au baada ya leba

 • Mtoto huwahi kushuka kwa ujauzito wa kwanza

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

1 Februari 2024 13:30:05

Rejea za mada hii

 1. What You Should Know About Head Engagement in Pregnancy. WebMDhttps://www.webmd.com/baby/head-engagement-in-pregnancy-what-is-it.  Imechukuliwa 06.01.2024

 2. How You Can Tell If Baby Is Engaged: Meaning, Symptoms, More. Healthline.  https://www.healthline.com/health/pregnancy/baby-engaged#signs-and-symptoms. Imechukuliwa 06.01.2024

bottom of page