Mwandishi:
Dkt. Adolf S, M.D
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, M.D
11 Julai 2023 10:47:56
Je, kuna njia mbadala za kuzuia ujauzito mbali na P2?
P2 hujulikana kama Levonorgestrel kwa jina la kijeneriki, hutumika kuzia ujauzito baada ya kushiriki ngono siku za hatari bila kinga.
Dawa hii imekuwa ikitumiwa sana katika kuzuia ujauzito, hata hivyo madhumuni ya dawa hii ni kuzuia ujauzito katika mazingira hatarishi tu. Mbali na P2 kuna dawa nyingine zinazotumika kuzuia ujauzito ambazo huwa maarufu kwa jina la vidonge vya majira ambavyo vip vya aina mbili kulingana na homoni iliyosanikishwa, vidonge hivyo ni;
Vidonge vya majira mchanganyiko
Vimetengenezwa kwa kusanikisha homoni progesterone na estrogen.
Vidonge vya majira vya progesterone
Vimetengenezwa kwa kusanikisha homoni progesterone tu.
Njia nyingine za uzazi wa mpango
Mbali na vidonge vya kuzuia mimba au vidonge vya majira, zifuatazo ni njia nyingine za uzazi wa mpango
Njia za asili kama vile kutumia kalenda, kunyonyesha na kumwaga mbegu nje
Kondomu ya kike
Kondomu ya kiume
Kipandikizi cha homoni
Kitanzi katika kizazi
Sindano ya homoni progesterone (DEPO Provera)
Kikombe cha shingo ya kizazi na dawa ya kuua mbegu za kiume
Kufunga mirija ya uzazi kwa mwanamke
Kufunga mirija ya uzazi kwa mwanaume
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
12 Julai 2023 19:31:52
Rejea za mada hii
Levonorgestrel – StatPearls – NCBI Bookshelf.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK539737/. Imechukuliwa 11.07.2023
Oral Contraceptive Pills – StatPearls – NCBI Bookshelf.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430882/. Imechukuliwa 11.07.2023
Overview of Contraception - Women's Health Issues - MSD Manuals.https://www.msdmanuals.com/home/women-s-health-issues/family-planning/hormonal-methods-of-contraception. Imechukuliwa 11.07.2023
STANDARD TREATMENT GUIDELINES AND NATIONAL ESSENTIAL MEDICINES LIST FOR TANZANIA MAINLAND. Sixth edition 2021. Pg 241-242.