Mwandishi:
Dkt Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, M.D
19 Julai 2023, 19:19:57

Je, unaweza PEP wakati unakunywa pombe?
Ndiyo, lakini haishauriwi.
Kilevi chochote kinachopatikana kama bia, spiriti, mvinyo, n.k huweza kutumiwa na mtu anayekunywa PEP kwa kiasi kinachoshauriwa kiafya kwa kuwa hakuna mwingiliano wa kimetaboli wa dawa hizo na pombe. hata hivyo haishauriwi sana kwa sababu zifuatazo:
Pombe hupunguza nidhamu ya kutumia dawa – Pombe inaweza kufanya usahau kunywa dozi yako kwa wakati unaofaa, jambo ambalo linaweza kupunguza ufanisi wa PEP.
Pombe hudhoofisha mfumo wa kinga – Matumizi ya pombe kwa kiasi kikubwa hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi, ambayo inaweza kuwa hatari wakati unapojaribu kuzuia VVU.
Pombe huongeza hatari ya kuonekana kwa maudhi ya dawa – Baadhi ya watu hupata maudhi kama kichefuchefu au maumivu ya kichwa wanapotumia PEP, matumizi ya PEP na pombe yanaweza kuzidisha maudhi haya kuwa ya kuonekana zaidi.
Wapi utapata maelezio zaidi?
Ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba pombe hupunguza ufanisi wa PEP, ni bora kuepuka au kupunguza unywaji wa pombe wakati wa kutumia dawa hizi ili kuhakikisha unapata matokeo mazuri. Kama una wasiwasi, ni vyema kushauriana na daktari wako.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
12 Machi 2025, 20:10:01
Rejea za mada hii
Alcohol and HIV. Aidsmap. https://www.aidsmap.com/about-hiv/alcohol-and-hiv. Imechukuliwa 18.07.2023
PEP. http://publichealth.lacounty.gov/dhsp/Biomedical/Basics_of_PEP_for_Patient-EN_12.29.2021.pdf. Imechukuliwa 18.07.2023